Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024

Yanga vs MC Alger Leo Saa Ngapi

Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 | Kikosi cha Yanga leo dhidi ya MC Alger Klabu Bingwa CAF

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions League), Yanga SC, leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuwakabili MC Alger ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kundi A. Mchezo huu utatoa majibu ya nani atafuzu hatua ya robo fainali, huku Yanga wakihitaji ushindi wowote ili kufanikisha ndoto yao.

Katika mechi ya awali iliyochezwa Algeria, Yanga walipoteza kwa mabao 2-0. Ushindi wa leo ni muhimu si tu kwa kulipiza kisasi bali pia kufanikisha hatua ya robo fainali kwa mara ya pili mfululizo, jambo ambalo litaweka historia ya kipekee kwa klabu hiyo.

MC Alger wapo nafasi ya pili kwenye kundi wakiwa na pointi nane, wakati Yanga wanashika nafasi ya tatu na pointi saba. Hii inamaanisha sare yoyote itawavusha wageni hao, lakini ushindi wa Yanga utawapa nafasi ya kuungana na Al Hilal kwenye hatua inayofuata.

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameweka wazi kuwa wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi muhimu. Kwa maneno yake, “Tunaelewa umuhimu wa mchezo huu. Tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao ni nguvu yetu. Tuna nidhamu ya hali ya juu na mbinu za kuhakikisha tunapata matokeo chanya.”

Nahodha wa timu, Dickson Job, alisisitiza kuwa wachezaji wapo tayari kupambana kwa ajili ya kuhakikisha wanawapa mashabiki furaha. “Hatuwezi kuruhusu makosa. Hii ni mechi muhimu sana kwa mustakabali wetu kwenye mashindano haya,” alisema.

Kwa upande wa wapinzani, MC Alger, kocha Khaled Benyahya, alisema timu yake imejipanga licha ya changamoto za hali ya hewa ya joto jijini Dar es Salaam. Pia, kikosi hicho kitapungukiwa baadhi ya wachezaji wao muhimu, kama Mohamed Zougrana na Merwane Khelif, ambao hawatacheza kwa sababu za kiafya.

Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024

Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024

Kikosi rasmi cha Yanga Sc kitakacho anza leo dhidi ya MC Alger kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa majira ya saa tisa jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.

Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024

Changamoto kwa Yanga

Licha ya maandalizi mazuri, Yanga itakosa huduma ya beki wa kulia Yao Kouassi, aliyeumia goti na kufanyiwa upasuaji. Hili linawapa Yanga changamoto ya kujipanga upya eneo la ulinzi, hasa dhidi ya mshambuliaji hatari wa MC Alger.

Zaidi ya hilo, Yanga wanapaswa kuwa makini na mbinu za MC Alger, kama kupoteza muda na kuchelewesha mchezo. Timu za Kaskazini mwa Afrika mara nyingi hutumia mbinu hizi hasa zinapokuwa ugenini.

Msimamo wa Kundi A

  • Al Hilal: Nafasi ya kwanza (Pointi 10)
  • MC Alger: Nafasi ya pili (Pointi 8)
  • Yanga: Nafasi ya tatu (Pointi 7)
  • TP Mazembe: Nafasi ya nne (Pointi 4)

Kwa Yanga, sare au kipigo leo kitawafanya waondolewe kwenye mashindano, wakati ushindi utawavusha kwenda robo fainali. Mchezo huu pia ni fursa kwa Yanga kulipa kisasi cha kichapo walichokipata Algeria.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 Saa Ngapi?
  2. Ligi 20 Bora Afrika 2025
  3. Yanga Wamejipanga Kupambana Kesho: Ramovic
  4. Kocha MC Alger Atamba Kupata Pointi 3 Dhidi ya Yanga Licha ya Joto Kali
  5. Ligi Kuu Bara Kurejea Februari kwa Moto! Simba na Yanga Kuanza na Viporo
  6. Mtibwa Sugar Kuwakaribisha Azam FC Manungu kwa Mechi ya Kirafiki
  7. Ligi Kuu Bara: JKT Tanzania Waitana Kambini, Kocha Apania Maboresho
  8. Watano Waagwa Azam Fc
  9. CV ya Jonathan Djogo Kapela: Winga Mpya wa Yanga SC
  10. Taifa Stars Yapangwa Kundi Laini CHAN 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo