Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025 | Kikosi cha Yanga leo Dhidi ya JKT Tanzania Ligi Kuu
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo watakuwa ugenini kumenyana na JKT Tanzania katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni jijini Dar Es Salaam. Mchezo huu ni wa mzunguko wa pili wa ligi kuu na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikiwa na malengo yake.
Kwa Yanga SC, ushindi katika mchezo huu ni muhimu ili kuendelea kuimarisha nafasi yao kileleni mwa msimamo wa ligi na kuongeza nafasi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Yanga SC kwa sasa wanashikilia nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 45 kutokana na michezo 17, wakiwa wameshinda mara 15 na kupoteza mara 2 pekee. Ushindi leo utawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa wao.
Kwa upande wa JKT Tanzania, mchezo huu ni muhimu katika jitihada zao za kubaki kwenye ligi kuu. Wakiwa na pointi 19 kutokana na michezo 17, wanahitaji matokeo mazuri ili kujiongezea matumaini ya kusalia. Mechi dhidi ya Yanga SC ni changamoto kubwa, lakini pia ni fursa kwao kuonyesha uwezo wao na kupunguza pengo la pointi dhidi ya timu zilizo juu yao.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa, huku Yanga SC wakitaka kuendeleza ubabe wao na JKT Tanzania wakipambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja. Ni mechi ambayo itatoa taswira kubwa ya hatima ya kila timu katika ligi kuu msimu huu.
Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
Kikosi rasmi cha Yanga kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9:00 alasiri. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Miloud Hamdi atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Yanga itaendelea kuimarisha nafasi yake kileleni, huku JKT Tanzania ikipambana kuendelea kujihimarisha katika nafasi za juu za msimamo wa ligi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025 Saa Ngapi?
- Bao la Kaseke Laipa Pamba Ushindi Dhidi ya Azam FC
- Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji Wampa Jeuri Minziro
- Ngassa: Mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini tunajua pakupenya
- KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate
- Ratiba ya Mechi za Tanzania (Taifa Stars) Afcon 2025
- CAF Yatangaza Ratiba Ya Fainali za Afcon 2025
- Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora
- Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
- Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
Leave a Reply