Kikosi cha Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi Dodoma Jiji
Yanga leo itashuka dimbani saa 10:00 jioni kucheza dhidi ya wenyeji wao, Dodoma Jiji FC, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga katika kampeni yao ya kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, wakilenga kulichukua kwa mara ya nne mfululizo. Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, ameweka wazi kuwa lengo lao kuu ni kushinda mechi hii na kuwapa mashabiki zawadi ya sikuu ya Krismasi.
Yanga inakuja kwenye mchezo huu ikiwa na rekodi nzuri msimu huu. Wameshinda michezo 11 kati ya 13 waliyocheza, wakifunga mabao 23 na kuruhusu mabao sita pekee. Timu hiyo, ambayo iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 33 sawa na Azam FC, ina matumaini ya kuongeza alama tatu muhimu ili kuimarisha nafasi yao ya kutwaa ubingwa.
Kocha Ramovic amesisitiza umuhimu wa kuwa makini katika mchezo huu, akitambua changamoto ya kucheza michezo mingi mfululizo. “Tumekuja Dodoma kwa lengo moja, kuchukua pointi tatu na kuwapa zawadi ya Krismasi mashabiki wetu,” alisema Ramovic.
Hata hivyo, mjerumani huyo amedokeza kuwa anaweza kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kutokana na uchovu wa wachezaji wake baada ya kucheza michezo miwili mfululizo dhidi ya Mashujaa FC na Prisons wiki iliyopita. Katika michezo hiyo, Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-2 na 4-0 mtawalia.
Dodoma Jiji FC, inayofundishwa na Mecky Maxime, itashuka dimbani ikijua fika ugumu wa mchezo huu. Timu hiyo iko nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza michezo 14. Mara ya mwisho Dodoma Jiji kupata ushindi ilikuwa Novemba 3, walipoifunga KenGold 1-0. Tangu wakati huo, wamejikuta wakipoteza mechi tatu na kutoka sare mara moja.
Kocha Maxime ameonya wachezaji wake dhidi ya kufanya makosa yasiyo ya lazima, akisema Yanga ni timu inayoweza kutumia makosa ya wapinzani wao kwa faida. “Timu kubwa kama Yanga zina uwezo wa kuadhibu makosa madogo madogo. Tunatakiwa kupunguza makosa na kufuata maelekezo ili kuwa na jioni nzuri kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Maxime.
Kikosi cha Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024
Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Dodoma Jiji kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.
Matarajio ya Mchezo
Mashabiki wa mpira wa miguu wanatarajia mechi yenye ushindani mkali kati ya timu hizi mbili. Kwa upande mmoja, Yanga inatafuta kuimarisha nafasi yao kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, huku kwa upande mwingine Dodoma Jiji ikilenga kutumia uwanja wake wa nyumbani kufufua matumaini yao ya kujiweka salama kwenye ligi.
Kwa wachezaji wa Yanga, mchezo huu ni nafasi nyingine ya kuthibitisha ubora wao, huku Dodoma Jiji wakipambana kuonyesha kuwa wanaweza kusimamisha mabingwa hao watetezi.
Mashabiki wanakaribishwa kushuhudia burudani hii ya mpira wa miguu, ikiwa ni moja ya michezo inayotarajiwa kuvutia hisia nyingi siku ya Krismasi. Je, Yanga itaendelea kung’ara au Dodoma Jiji watawazuia mabingwa hawa? Muda utaamua.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Penati ya Dakika za Majeruhi Yaipa Simba Pointi Tatu Dhidi ya JKT
- Matokeo ya Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024
- Shaban Chilunda Awindwa na KMC
- Yanga Yaibuka na Pointi tatu Dhidi ya Tanzania Prisons
- Vita ya Kumsajili Okoyo Yazuka Kati ya KMC, Mashujaa na Namungo
- Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars
Leave a Reply