Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 14/09/2024

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 14/09/2024 | Kikosi cha Yanga Leo Vs CBE SA Klabu Bingwa

Leo hii, mashabiki wa soka nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wanatarajia mechi kubwa kati ya Yanga SC, mabingwa wa Tanzania, dhidi ya CBE SA ya Ethiopia. Mchezo huu wa raundi ya kwanza, mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF, utaanza rasmi majira ya saa 9:00 mchana katika uwanja mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia. Hii ni moja ya mechi muhimu kwa Yanga katika harakati zao za kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa kwa mara ya pili mfululizo.

Yanga inakutana na CBE SA ikiwa na wachezaji wake wote wakiwa salama baada ya kumaliza majukumu yao ya kimataifa. Timu ilipata maandalizi ya kutosha licha ya changamoto ya safari, ambapo wachezaji walitoka kwenye majukumu ya timu za taifa moja kwa moja kuelekea Addis Ababa kupitia ndege za Shirika la Ndege la Ethiopia. Ushirikiano wa viongozi wa Yanga kuhakikisha kuwa kila mchezaji anaingia kambini kwa wakati, umewapa timu hiyo nguvu na umoja kuelekea mchezo huu muhimu.

CBE SA ni timu ambayo imepata mafanikio makubwa kwa haraka. Timu hiyo inayomilikiwa na Benki ya Biashara ya Ethiopia ilijijenga upya mnamo mwaka 2021 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia baada ya kupanda daraja msimu uliopita.

Katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF, CBE iliing’oa SC Villa ya Uganda kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2, ikishinda ugenini 2-1 na kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa nyumbani.

Licha ya kuwa na wachezaji wachache wa kigeni, kama vile beki wa Ghana Caleb Amankwah na kiungo Umar Bashiru, pamoja na mshambuliaji kutoka Uganda Simon Oketch, CBE imejipanga vizuri na wanategemea uwezo wa wachezaji wao wa ndani pamoja na mbinu bora za kiufundi ili kushinda mechi hii.

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 14/09/2024

Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 14/09/2024

Katika mchezo huu muhimu wa Yanga dhidi ya CBE SA, matarajio ni makubwa kwa mashabiki wa Yanga. Wengi wanatamani kuona kikosi bora zaidi cha Yanga kikipambana uwanjani ili kuhakikisha ushindi wa mapema. Kocha Miguel Gamondi anatarajiwa kutangaza rasmi kikosi kitakachoanza majira ya saa nane mchana, na tutakuwa hapa kukuletea orodha kamili.

Kikosi Rasmi cha Yanga Kinachoanza Leo Dhidi ya CBE (Starting XI):

  • Diarra (39)
  • Boka (23)
  • Job (5)
  • Muamnyeeto (3) (Captain)
  • Bacca (4)
  • Aucho (8)
  • Maxi (7)
    Mudathir (27)
  • Dube (29)
  • Aziz Ki (10)
  • Pacome (26)

Subs: Mshery, Yao, Andabwile, Mkude, SureBoy, Abuya, Chama, Mzize & Baleke

Kikosi cha Yanga leo dhidi ya CBE

Huku tukisubiri tangazo rasmi, Habariforum imeandaa utabiri wa kikosi kinachoweza kuanza leo, kwa kuzingatia ubora na hali ya sasa ya wachezaji:

Kikosi cha Yanga Kinachotarajiwa Dhidi ya CBE SA(4-3-3)

  • Kipa: Diarra
  • Mabeki: Yao, Bakari Nondo, Job, Bacca
  • Viungo: Aucho, Mudathir, Aziz Ki
  • Washambuliaji: , Mzize, Max Mpia, Pacome

Mfumo huu wa 4-3-3 unalenga kuimarisha safu ya ulinzi huku ukiacha nafasi kwa washambuliaji wenye kasi kushambulia kwa nguvu.

Rekodi za Yanga Dhidi ya Timu za Ethiopia

Yanga inakutana na CBE ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zao za awali kwa kishindo. Katika raundi ya kwanza, Yanga iliirarua Vital’O ya Burundi kwa jumla ya mabao 10-0, hivyo kuonesha wazi nia yao ya kuandika historia nyingine kwa msimu huu. Hata hivyo, Yanga inatambua changamoto iliyopo, kwani mara ya mwisho kucheza nchini Ethiopia mwaka 2018, walipoteza 1-0 dhidi ya Welayta Dicha. Hii inawapa Yanga changamoto ya kuvunja mwiko huo wa kutopata ushindi nchini Ethiopia.

Matarajio ya Mechi ya Leo

Kwa upande wa Yanga, mkakati ni kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika uwanja wa ugenini. Timu zote mbili zinafahamika kwa kucheza soka la kushambulia, hivyo mashabiki wanatarajia mchezo wa kuvutia ambao utakuwa na ushindani mkubwa. Wakati CBE ikiwa na hamu ya kuandika historia mpya ya kufika hatua ya makundi, Yanga inataka kuimarisha nafasi yao ya kusonga mbele na kufanikisha lengo lao la kufika robo fainali tena msimu huu.

Mbinu za Yanga zitategemea wachezaji wao nyota kama Stephan Aziz Ki, Pacome Zouzoua, na Ibrahim Bacca, ambao wamekuwa nguzo muhimu msimu huu. Kwa upande wa CBE, wachezaji wao wa kigeni pamoja na uwezo wa kumiliki mpira, wanaweza kutoa changamoto kubwa kwa Yanga.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jeuri ya Simba Kombe la Shirikisho CAF ipo Hapa
  2. Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu
  3. Goli Pekee la Ngushi Laipa Mashaujaa Ushindi Dhidi ya Coastal Union
  4. Nani Atashinda Ballon d’Or 2024? Rodri, Vinicius Jr, Au Jude Bellingham?
  5. Yanga Vs CBE SA: Saa Ngapi Mechi Inaanza?
  6. Lawi Ndani ya Kikosi cha Coastal Union Dhidi ya Mashujaa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo