Kikosi cha Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024 | Kikosi cha Yanga leo Vs Al Hilal Klabu Bingwa CAF
Timu ya wananchi, Yanga SC, leo itashuka dimbani kuanza safari ya kuitetea Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga itakutana na Al Hilal ya Sudan katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na mvuto wa aina yake, ukiwa sehemu ya hatua ya makundi ya michuano hiyo. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni.
Katika makala hii, tutazama kwenye historia ya timu zote mbili, rekodi zao kwenye michuano ya CAF, maandalizi ya kila kikosi na orodha ya wachezaji watakaounda kikosi cha kwanza cha Yanga na matarajio ya mchezo huu unaosubiliwa na mashabiki wengi wa soka Afrika.
Kwa mara ya pili mfululizo, Yanga imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Msimu uliopita, ilifika robo fainali na kuondolewa na Mamelodi Sundowns kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Rekodi za Yanga zinaonyesha kuwa ni timu ngumu inapocheza nyumbani. Katika misimu miwili iliyopita, Yanga imepoteza mchezo mmoja tu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.
Kwa msimu huu, Yanga imetinga makundi kwa ushindi mkubwa katika hatua za mtoano. Iliifunga Vital’O ya Burundi kwa jumla ya mabao 10-0 na kisha ikaishinda CBE ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-0. Yanga haijaruhusu bao lolote kufungwa katika mechi hizo, ikionyesha uimara wake wa kiulinzi na mashambulizi makali.
Al Hilal ni moja ya timu zenye rekodi nzuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Timu hii imecheza fainali mbili, mwaka 1987 na 1992, na kufika nusu fainali mara tano. Pia, Al Hilal imewahi kufika hatua ya makundi mara nane, ikionyesha uzoefu wa hali ya juu katika mashindano haya.
Katika hatua za mtoano msimu huu, Al Hilal iliifunga Al Ahly Benghazi ya Libya kwa jumla ya mabao 2-1 na kisha kuiondoa San Pedro ya Ivory Coast kwa mabao 3-2. Timu hii inajivunia safu bora ya ushambuliaji na ulinzi madhubuti.
Kikosi cha Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024
Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Al Hilal kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.
Kocha mpya wa Yanga, Sead Ramovic, anaingia kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya CAF akiwa kocha wa timu hiyo. Ramovic, aliyeteuliwa Novemba 15, 2024, anatarajiwa kuendeleza rekodi nzuri ya Yanga ya kufika hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo, jambo ambalo lilifanikishwa awali na kocha Miguel Gamondi.
Kwa upande mwingine, kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge, anakutana tena na changamoto ya kucheza Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao umekuwa ukiwanyima ushindi mara kadhaa katika historia yake ya ukocha.
Matarajio ya Mchezo Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa. Rekodi za timu zote zinaonyesha kwamba kila moja ina uwezo wa kupindua matokeo, lakini faida ya kucheza nyumbani inaweza kuwa silaha ya ziada kwa Yanga. Wakati Yanga inajivunia mashabiki wake wa nyumbani na historia nzuri kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Al Hilal inakuja na uzoefu mkubwa wa kushindana katika viwanja vya ugenini.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Rekodi za Refa Atakaye Chezesha Mechi ya Yanga vs Al Hilal
- Ratiba ya Mechi za leo 26/11/2024
- Mechi ya Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024 Saa Ngapi?
- Yanga Tayari kwa Vita ya CAF: Ramovic Afunguka
- Yanga Uso Kwa Uso na Copco Kombe la FA
- Ratiba ya Kombe la Shirikisho la CRDB 2024/2025
- Simba SC Yavunja Mkataba na CEO Francois Regis
- Kocha Minziro Afurahishwa na Uchezaji wa Pamba Jiji, Aahidi Matokeo Bora
- Ken Gold Walazimisha Sare Dhidi ya Coastal Union Sokoine
Leave a Reply