Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025

Al Hilal VS Yanga Leo Saa Ngapi

Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Al Hilal Klabu Bingwa CAF

Leo Ndio Leo kwa Yanga SC! Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Yanga SC, wanashuka dimbani kumenyana na Al Hilal ya Sudan katika mchezo muhimu wa kuisaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa leo saa 4:00 usiku, ukiwa na uzito mkubwa kwa Yanga ambao wanahitaji alama tatu muhimu ili kujihakikishia nafasi nzuri zaidi ya kuendelea mbele kwenye kundi lao.

Kocha wa Yanga, Sead Ramovic, ameweka wazi kuwa maandalizi yao yamelenga kuhakikisha ushindi wa ugenini. Ramovic anasisitiza umuhimu wa kuimarisha kikosi chake badala ya kuangalia wapinzani wanavyocheza. Katika mahojiano yake, alisema:

“Simuangalii mpinzani ili kuwa bora. Ninapambana kuhakikisha tunakuwa washindani kwa kuboresha kikosi changu. Tuna morali nzuri, na naamini tunaweza kushinda kwa kushindana sisi wenyewe.”

Kwa sasa Yanga inashika nafasi ya tatu katika kundi A ikiwa na alama nne, huku Al Hilal tayari wakiwa wamefuzu wakiwa na alama 10. Ushindi wa Yanga leo utawapeleka hadi alama saba, jambo litakalowafanya kubakia nyuma ya MC Alger kwa tofauti ya alama moja, ikiwa MC Alger itashinda mechi yake dhidi ya TP Mazembe.

Ulazima wa ushindi kwa Yanga unazidi kushika kasi kutokana na matokeo ya MC Alger, ambayo ilishinda dhidi ya TP Mazembe kwa bao 1-0 hivi karibuni. Ushindi wa leo utaipa Yanga nafasi nzuri ya kuamua hatma yao katika mechi ya mwisho dhidi ya MC Alger itakayofanyika kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Januari 18.

Kwa upande wa Al Hilal, kocha Florent Ibenge ameonyesha dhamira ya kutoweka presha kubwa kwa wachezaji wake wakuu, akieleza kuwa wanapanga kutumia mechi hizi mbili zilizobaki kama maandalizi ya robo fainali. “Hatuwezi kuonyesha kiburi mapema. Tunapumzisha baadhi ya mastaa wetu kwa ajili ya hatua zijazo,” alisema Ibenge.

Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025

Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025

Kikosi rasmi cha Yanga Sc kitakacho anza leo dhidi ya Al Hilal kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa majira ya saa tatu usiku. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.

Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025

Wachezaji wa Kuangaliwa Leo

Kwa Yanga, mchezaji wa kiungo Pacome Zouzoua ameonyesha kiwango cha juu katika hatua ya makundi, akitengeneza nafasi nane za kufunga, ingawa bado hazijazalisha mabao. Ushirikiano wake na nyota wengine kama Clatous Chama na mshambuliaji Clement Mzize, ambaye tayari ana mabao matano, unatarajiwa kuwa silaha kubwa kwa Yanga leo.

Kwa Al Hilal, licha ya kuwa wamefuzu, uzoefu wao wa michuano ya Afrika unawapa nguvu ya kuonyesha upinzani mkali dhidi ya Yanga. Wana rekodi nzuri ya kumaliza hatua ya makundi kwa mafanikio, hivyo Yanga wanapaswa kuwa makini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Leo 12/01/2025
  2. Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
  3. Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
  4. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  5. Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
  6. AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
  7. Walioitwa Kwenye Usaili Uhamiaji 2025
  8. Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
  9. Robert Matano Ateuliwa Kuwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate FC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo