Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024

MC Alger Vs Yanga Leo Saa ngapi

Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024 | Kikosi cha Yanga leo Dhidi ya MC Alger Klabu Bingwa

Yanga SC inatarajiwa kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Desemba 7, 2024, dhidi ya MC Alger kwenye Uwanja wa Julai 5, 1962, mjini Algiers. Mchezo huu ni muhimu kwa Yanga, ambayo imepewa nafasi kubwa ya kupata matokeo mazuri kutokana na takwimu dhaifu za wapinzani wao wakiwa nyumbani.

MC Alger imekuwa na matokeo ya kutia shaka kwenye Ligi Kuu ya Algeria, ambapo kwa jumla imecheza michezo kumi, ikiwa imeshinda minne, imetoka sare mitano, na kufungwa mara moja. Matokeo mabaya zaidi kwao yanatokana na michezo yao ya nyumbani.

Katika mechi tano zilizochezwa nyumbani, MC Alger imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare tatu, na kupoteza mmoja, hivyo kukusanya jumla ya pointi sita tu kati ya 15 zinazowezekana. Pia katika michezo ya nyumbani, MC Alger imefunga mabao matatu pekee, huku ikiruhusu mabao manne. Hali hii ni tofauti kabisa na matokeo ya ugenini, ambapo wameweza kufunga mabao matano na kuruhusu mabao mawili. Kwa jumla, MC Alger imefunga mabao nane na kuruhusu mabao sita. Hii inadhihirisha udhaifu wa timu hii katika kujilinda wakati wanacheza mbele ya mashabiki wao, jambo ambalo Yanga inaweza kulichukua kama fursa muhimu.

Yanga SC imejiandaa kuingia katika mchezo huu ikiwa na kikosi kilichokamilika na wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa. Uwepo wa wachezaji muhimu kama Stephan Aziz Ki na Pacome Zouzoua, ambao wameonyesha kiwango cha juu katika michuano ya Afrika, ni faida kubwa kwa timu hii. Aidha, Yanga imeweza kusajili wachezaji bora na kuimarisha kikosi chake msimu huu, hivyo kuwa na uwezo wa kupambana na timu yoyote kubwa barani Afrika.

Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024

Kikosi cha Yanga SC vs MC Alger Leo 7/12/2024

Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya MC Alger kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tatu usiku. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Sead Ramovic.

Kikosi cha Yanga kinachoanza leo dhidi ya MC Alger

  1. Diarra (39)
  2. Yao (21)
  3. Kibabage (30)
  4. Mwamyeto (3) (Captain)
  5. Bacca (4)
  6. Abuya (38)
  7. Maxi (7)
  8. Mudathir (27)
  9. Musonda (25)
  10. Aziz Ki (10)
  11. Pacome (26)

Wachezaji wa Ziada: Khomeiny, Kibwana, Nkane, Mkude, Aucho, Shekhan, Chama, Farid, Dube

Kocha Mkuu: Sead Ramovic

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. MC Alger Vs Yanga Leo 07/12/2024 Saa ngapi?
  2. Kikosi cha Yanga Tayari kwa Vita ya Algiers
  3. Fei Toto Aendelea Kuwaka Ligi Kuu, Anaongoza kwa Mabao na Assists
  4. Coastal waweka wazi mpango wa kutinga Nne bora Ligi Kuu
  5. Chikola Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Novemba
  6. Ratiba ya Simba Sc December 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo