Kikosi Cha Yanga 2024/2025 | Majina ya Wachezaji Wote Wa Yanga
Katika msimu wa 2023/2024, Yanga SC imefanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania ya NBC kwa kumaliza kileleni mwa msimamo wa ligi kwa jumla ya pointi 80 katika michezo 30, wakiwa wameshinda michezo 26, wametoa sare michezo 2, na wamefungwa michezo miwili. Pia, Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho, ambalo linafahamika pia kama CRDB Bank Federation Cup, baada ya kuifunga Azam kwa mikwaju ya penati.
Mbali na mafanikio haya katika mashindano ya ndani ya Tanzania, Yanga SC pia iliweza kuheshimisha soka la Tanzania baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya kimataifa, licha ya kutolewa na Mamelodi Sundowns katika hatua hiyo. Mafanikio haya yameweka msingi mzuri kwa timu kuelekea msimu wa 2024/2025, ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na changamoto nyingi.
Katika makala hii, tutaangazia kikosi cha Yanga msimu wa 2024/2025, wachezaji muhimu kutokana na nafasi wanazocheza. Kama wewe ni shabiki wa Yanga basi chapisho hili linakupa nafasi ya kujua majina ya wachezaji wa Yanga 2024/2025 pamoja na nafasi wanazocheza.
Wachezaji Muhimu Wa Yanga kwa Msimu wa 2024/2025
Katika msimu wa 2024/2025, Yanga SC inatarajia kutegemea wachezaji wake muhimu ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika misimu iliyopita na wale wapya waliojiunga na kikosi. Wachezaji hawa ni Stephan Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, na Ibrahim Bacca.
Stephan Aziz Ki
Stephan Aziz Ki ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali katika uwanja wa kati. Ana sifa ya kumiliki mpira vizuri, kutoa pasi sahihi, na uwezo mkubwa wa kudhibiti kasi ya mchezo. Uwezo wake wa kiufundi na uzoefu wake utakuwa muhimu sana kwa Yanga SC katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri msimu huu.
Pacome Zouzoua
Pacome Zouzoua ni mchezaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabao. Akiwa na sifa za mshambuliaji wa kisasa, Zouzoua ni tishio kwa safu yoyote ya ulinzi na aliweza kuonesha hilo katika msimu wa 2023/2024. Uwezo wake wa kumalizia na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji utakuwa na faida kubwa kwa Yanga SC msimu huu.
Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli ni kiungo mkabaji mwenye nguvu na uwezo wa kuzuia mashambulizi ya wapinzani. Nzengeli ana sifa ya kuwa na nidhamu nzuri ya uchezaji, uwezo wa kushinda mipira ya juu, na kasi ya kuzuia na kupandisha mashambulizi ya haraka. Kwa ushirikiano mzuri na mabeki wengine, anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga SC na pia kua kiungo kikukwa jikoni mwa Yanga Sc.
Ibrahim Bacca
Ibrahim Bacca ni beki wa kati mwenye nguvu na uwezo wa kusoma mchezo vizuri. Bacca ana sifa ya kuwa na uwezo wa kuzuia mashambulizi ya wapinzani kwa umakini, kushinda mipira ya hewani, na kutoa msaada kwa mabeki wenzake. Uwepo wake katika safu ya ulinzi ni muhimu kwa kuimarisha kikosi na kuhakikisha timu inabaki imara nyuma.
Kikosi Cha Yanga 2024/2025 | Majina ya Wachezaji Wote Wa Yanga
MAGOLIKIPA
- Djigui Diarra
- Erick Johola
- Abdultwalik Msheri
MABEKI
- Djuma Shaban
- Kibwana Shomari
- David Bryson
- Joyce Lomalisa
- Abdallah Shaibu
- Dickson Job
- Bakari Nondo
- Yanick Bangala
- Ibrahim Bacca
VIUNGO
- Khalid Aucho
- Gael Bigirimana
- Aziz Ki Stephane
- Feisal Salum
- Zawadi Mauya
- Farid Mussa
- Jesus Moloko
- Dickson Ambundo
- Salum Aboubakary Sure Boy
- Denis Nkane
- Benard Morrison
WASHAMBULIAJI
- Fiston Mayele
- Yusuph Athuman
- Chrispin Ngush
- Yacouba Sogne
- Heritier Makambo
- Lazarous Kambole
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
- Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024
- Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024
- Hiki Apa Kikosi Cha Taifa Stars Kitakacho Cheza Na Sudan Mechi za Kirafiki 2024
- FIFA Yaiondolea Yanga Adhabu ya Kufungiwa Kusajili
- Wachezaji Walio Ongeza Mkataba Simba 2024/2025
- Taarifa Rasmi: Simba Yatangaza Kuachana na Henock Inonga
- Tuisila Kisinda Atajwa Kutakiwa Coastal Union 2024/2025
Leave a Reply