Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024

Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024 | Kikosi Cha Ureno (Portugal) Kwaajili ya Michuano ya EURO 2024

Kocha mkuu wa Ureno Roberto Martinez ametangaza kikosi rasmi cha Ureno kitakachochuana vikali katika michuano mikubwa ya Euro 2024 nchini Ujerumani. Mashabiki wa soka kote duniani wanasubiri kwa hamu kuona kama Ureno, mabingwa wa Euro 2016, wataweza kurudia mafanikio hayo makubwa haswa kutokana na nyota wao Ronaldo aliesaidia kwa kiwango kikubwa mwaka 20216 kupungua makali.

Jambo lililowavutia mashabiki wengi ni uwepo wa Cristiano Ronaldo, mchezaji nyota ambaye amekuwa akipeperusha vyema bendera ya Ureno kwa miaka mingi. Licha ya umri wake wa miaka 39 na kucheza ligi ya Saudi Arabia, Ronaldo bado ni mshambuliaji hatari mwenye rekodi nzuri ya kutia mpira nyavuni mara nyingi katika mashindano haya. Je, hii itakuwa michuano yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa?

Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024

Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024

Kikosi cha Ureno kilichotangazwa kimejaa vipaji vinavyong’ara kutoka ligi mbalimbali duniani, hasa Ligi Kuu England. Majina makubwa kama Ruben Dias, Bruno Fernandes, Diogo Jota, na Bernardo Silva yanaonesha nia ya Ureno kuleta ushindani mkali katika Euro 2024.

Katika safu ya ulinzi, Pepe, beki mkongwe wa Porto, anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuchaguliwa kwa michuano ya Euro. Uwepo wake pamoja na wachezaji wengine mahiri kama Ruben Dias, Joao Cancelo, na Nuno Mendes unathibitisha kuwa Ureno ina ukuta mgumu wa kuupenya.

Kiungo cha Ureno kitaongozwa na Bruno Fernandes, mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kusambaza pasi za mabao na kufunga mwenyewe. Wachezaji wengine kama Joao Palhinha, Ruben Neves, na Vitinha wanaongeza nguvu na umahiri katika eneo hili muhimu la uwanja.

Wakati Ronaldo akiwa kivutio kikubwa, kikosi cha Ureno kimejumuisha vijana wenye kasi na uwezo wa kufunga mabao, kama Goncalo Ramos, Joao Felix, na Rafael Leao. Hii inaleta changamoto ya kuona nani atakayeongoza safu ya ushambuliaji na kuisaidia Ureno.

Hiki ndicho Kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Euro 2024

Makipa: Diogo Costa (FC Porto), José Sá (Wolverhampton Wanderers FC) e Rui Patrício (AS Roma);

Mabeki: António Silva (SL Benfica), Danilo Pereira (PSG), Diogo Dalot (Manchester United), Gonçalo Inácio (Sporting CP), Joao Cancelo (FC Barcelona), Nélson Semedo (Wolverhampton Wanderers), Nuno Mendes (PSG), Pepe (FC Porto), Rúben Dias (Manchester City

Viungo: Bruno Fernandes (Manchester United), Joao Neves (SL Benfica), João Palhinha (Fulham FC), Otávio Monteiro (Al Nassr), Rúben Neves (Al-Hilal), Vitinha (PSG)

Washambuliaji: Bernardo Silva (Manchester City), Cristiano Ronaldo (Al Nassr), Diogo Jota (Liverpool FC), Francisco Conceição (FC Porto), Goncalo Ramos (PSG), Joao Felix (FC Barcelona), Pedro Neto (Wolverhampton Wanderers), Rafael Leao (AC Milan).

Michezo ya Kujipima Nguvu Kabla ya Euro 2024

Kabla ya kuanza kwa michuano ya EURO 24 rasmi, Ureno imepanga kucheza michezo mitatu ya kujipima nguvu dhidi ya Finland, Croatia, na Jamhuri ya Ireland. Michezo hii itakuwa muhimu kwa kocha Martinez kujaribu mbinu zake na kuona ni wachezaji gani watakuwa katika kiwango bora zaidi kuelekea Ujerumani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Orodha Kamili ya Makombe na Tuzo za Toni Kroos
  2. Timu zilizowahi Kumaliza Msimu Bila Kufungwa
  3. Yanga SC Kusherehekea Ubingwa wa Ligi kwa Parade Kubwa Mei 25
  4. Tuzo za Ligi Kuu England 2023/24: Hawa Apa washindi wa Tuzo EPL
  5. Liverpool Yamtambulisha Arne Slot Kama Kocha Mpya Rasmi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo