Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea 10 September 2024

Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea 10 September 2024 | Kikosi cha Taifa Stars Vs Guinea AFCON

Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, itakutana na Guinea katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro, Ivory Coast jumanne ya tareh 10 septemba 2024.

Taifa Stars itaingia kwenye mchezo huu ikiwa na malengo ya kupata alama tatu muhimu ili kujiweka vizuri zaidi kwenye nafasi za kufuzu michuano hiyo mikubwa ya bara Afrika.

Kikosi cha Taifa Stars kiliondoka nchini Tanzania kuelekea Ivory Coast tayari kwa ajili ya mtanange huu muhimu. Kocha mkuu wa muda, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ameweka wazi kuwa kikosi kimefanya maandalizi ya kutosha na kimejipanga kuhakikisha kinaondoka na ushindi kwenye mchezo huu wa ugenini. Akizungumzia maandalizi yao, kocha Morocco alisema:

“Baada ya sare dhidi ya Ethiopia, tulifanya tathmini ya kikosi na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Tumefanyia kazi suala la umaliziaji ambalo lilituumiza kwenye mchezo uliopita, na sasa tupo tayari kwa changamoto dhidi ya Guinea.”

Tanzania inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na alama moja baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Ethiopia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku Guinea ikitoka kupoteza dhidi ya DR Congo kwa bao 1-0.

Mara ya mwisho kwa Taifa Stars kukutana na Guinea ilikuwa Januari 2021, kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) ambapo walitoka sare ya 2-2. Katika mchezo huo, Baraka Majogoro na Edward Manyama walifunga mabao kwa upande wa Tanzania. Hii inaashiria kuwa Taifa Stars ina uwezo wa kutoa ushindani dhidi ya Guinea, ingawa mchezo wa Septemba 10 utakuwa na presha zaidi kwa sababu ni wa kuwania nafasi ya kufuzu AFCON 2025.

Novatus Dismas, kiungo mkabaji wa Taifa Stars, amesema kuwa wachezaji wote wako tayari kwa changamoto hii na hawana presha dhidi ya Guinea. Dismas aliongeza kuwa dhamira yao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu wa ugenini.

Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea 10 September 2024

Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea 10 September 2024

Kikosi rasmi cha Taifa Stars vs Guinea kitakacho cheza katika tarehe 10 September 2024 kinatarajiwa kutangazwa siku ya mechi lisaa kabla ya mwamuzi wa mchezo kupuliza kipenga cha kuanzisha kabumbu. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi cha Tanzania mara tu baada ya kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kukitangaza.

Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea

Kikosi Kinachotarajiwa cha Taifa Stars

Taifa Stars ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko uwanjani, na kocha Morocco anatarajia kuwategemea baadhi ya wachezaji muhimu waliopo kwenye kikosi chake. Baadhi ya wachezaji wa msingi wanaotarajiwa kuanza kwenye mchezo huu ni:

  • Novatus Dismas – Kiungo mwenye nguvu na uwezo wa kuchezesha timu.
  • Clement Mzize – Mshambuliaji mwenye kasi na umakini wa kufunga.
  • Feisal Salum – Kiungo mwenye uwezo wa kusambaza mipira na kuanzisha mashambulizi.
  • Kelvin Barua – Mshambuliaji tegemeo mwenye uzoefu wa kimataifa.
  • Mudathir Yahya

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Wachezaji wa Kike wa Tanzania Wanaocheza Mpira Nje ya Nchi 2024
  2. Simba yaeka Marengo Ya CAF, Mo Dewji Arejea Kuongoza Mikakati
  3. CV ya Kocha Mpya Wa Azam Rachid Taoussi
  4. Serengeti Girls Waibuka Mabingwa Kombe la UNAF U17 Tunisia 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo