Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Kikosi cha timu ya Taifa

Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 | Wachezaji walioitwa Taifa star 2024 | Kikosi cha Taifa Stars 2024/2025

Kikosi cha Taifa Stars, chini ya Kaimu Kocha Mkuu Hemed Suleiman, kimetajwa rasmi kuanza maandalizi kwa ajili ya michezo miwili muhimu ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Maandalizi haya ni sehemu muhimu ya mkakati wa timu ya Taifa Stars kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Kocha Hemed Suleiman ameteua wachezaji 23 ambao wataingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Ethiopia na Guinea. Michezo hiyo itachezwa tarehe 4 Septemba na 10 Septemba 2024, ikiwa na umuhimu mkubwa katika safari ya kufuzu katika michuano ya AFCON 2025 ambayo inatarajiwa kufanyika Morocco.

Kikosi hiki kimejumuisha wachezaji wenye vipaji na uzoefu kutoka klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Wachezaji wa Yanga SC na Simba SC wakiwa na wawakilishi wengi, huku pia kukiwa na wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania kama Himid Mao anayekipiga Tala’a El Geish ya Misri na Cyprian Kachwele anayechezea Vancouver Whitecaps nchini Canada.

Angalia Hapa Kikosi cha Tanzania Taifa Stars Vs Dr Congo leo 10-10-2024

Angalia Hapa Kikosi cha Tanzania Vs Ethiopia 16/11/2024

Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Orodha ya wachezaji walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

  1. Ally Salim – Simba SC
  2. Abdultwalib Mshery – Young Africans
  3. Yona Amos – Pamba SC
  4. Lusajo Mwaikenda – Azam FC
  5. Nathaniel Chilambo – Azam FC
  6. Mohamed Hussein – Simba SC
  7. Dickson Job – Young Africans
  8. Pascal Msindo – Azam FC
  9. Ibrahim Hamad – Young Africans
  10. Bakari Nondo – Young Africans
  11. Nickson Kibabage – Young Africans
  12. Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
  13. Adolf Mtasigwa – Azam FC
  14. Himid Mao – Tala’a El Geish, Misri
  15. Novatus Dismas – Goztepe, Uturuki
  16. Mudathir Yahya – Young Africans
  17. Hussein Semfuko – Coastal Union
  18. Edwin Balua – Simba SC
  19. Feisal Salim – Azam FC
  20. Wazir Junior – Dodoma Jiji
  21. Cyprian Kachwele – Vancouver Whitecaps, Canada
  22. Clement Mzize – Young Africans
  23. Abel Josiah – TDS TFF Academy
Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
Kikosi cha Taifa Stars 2024/2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025
  2. Tabora united Yaibuka na Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Namungo
  3. Ratiba Ya Simba Kombe la Shirikisho CAF Confederation Cup 2024/2025
  4. Ifahamu CBE SA Ya Ethiopia Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa
  5. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  6. Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024
  7. Yanga Kucheza na CBE SA Ya Ethiopia Klabu Bingwa Septemba 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo