Kikosi cha Taifa Star Kilichoitwa Kambini Kufuzu Kombe la Dunia
Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kilichoitwa na kocha Hemed Morocco kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Morocco kimewekwa wazi. Mechi hiyo itapigwa Machi 26, 2025, huku Tanzania ikitarajia kufanya maandalizi makali kuhakikisha inapata matokeo mazuri ugenini.
Katika kikosi kilichoitwa, nyota mbalimbali kutoka klabu za ndani na nje ya nchi wamejumuishwa. Hata hivyo, nahodha Mbwana Samatta hajajumuishwa kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa majeruhi.
Walinda Mlango:
- Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)
- Ally Salim (Simba SC)
- Hussein Masaranga (Singida BS)
Mabeki:
- Shomari Kapombe (Simba SC)
- Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
- Mohamed Hussein (Simba SC)
- Pascal Msindo (Azam FC)
- Mirajy Abdallah (Coastal Union)
- Ibrahim Abdulla (Young Africans)
- Dickson Job (Young Africans)
- Abdulrazack Mohamed (Simba SC)
Viungo:
- Ibrahim Ame (Mashujaa FC)
- Jahi Mnoga (Salford City, Uingereza)
- Novatus Miroshi (Göztepe FC, Uturuki)
- Mudathir Yahya (Young Africans)
- Yusuph Kagoma (Simba SC)
- Feisal Salum (Azam FC)
- Charles M’Mombwa (Newcastle United Jets, Australia)
Washambuliaji:
- Kibu Denis (Simba SC)
- Simon Msuva (Al-Talaba SC, Iraq)
- Clement Mzize (Young Africans)
- Iddy Selemani (Azam FC)
- Selemani Mwalimu (Wydad Casablanca, Morocco)
- Kelvin John (Aalborg BK, Denmark)
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply