Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024

Simba Vs Yanga Sc Leo 19 10 2024 Saa Ngapi

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024 | Kikosi cha Simba leo Vs Yanga ligi Kuu | Kikosi cha Simba Dhidi ya Yanga

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo watashuka dimbani kuwakalibisha mahasimu wao wa jadi, Yanga SC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo huu, unaotarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, umevuta hisia za mashabiki wengi kutokana na upinzani mkali wa timu hizi mbili zinazoshika nafasi za juu katika soka la Tanzania.

Kariakoo Dabi imekuwa mechi ya kipekee kila msimu, huku mashabiki wa pande zote mbili wakiwa na matarajio makubwa ya kuondoka na alama tatu muhimu. Simba SC, ambao msimu huu wa 2024/25 hawajapoteza mchezo wowote wa ligi, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na ari ya kuimarisha nafasi yao ya ushindani. Kocha wao, Fadlu Davids, ameweka wazi kwamba hawana hofu na wanajiandaa kwa ushindani mkali. “Tunakwenda uwanjani kwa ajili ya msako wa pointi tatu. Maandalizi yetu yameanza muda mrefu, wachezaji wetu wapo fiti na tumejipanga vilivyo,” alisema Ahmed Ally, Afisa Habari wa Simba SC.

Ahmed Ally, Afisa Habari wa Simba, alizungumza kwa kujiamini juu ya maandalizi ya timu yake, akisema kuwa wanakwenda kuwashinda Yanga kwa mpango wa ‘Tripple Frontier’. “Tutawapiga mapigo matatu makubwa, kwanza Pumzi ya moto, pili tutawakaanga, na mwisho tutamalizia na Ubaya ubwela,” alisema Ally, akionyesha ari kubwa ya kuipatia Simba ushindi katika mchezo wa leo.

Huku Yanga wakitarajia kuimarisha uongozi wao kwenye ligi, Simba wanaonekana kuwa na shauku ya kupata ushindi na kuonesha ubora wao mbele ya maelfu ya mashabiki watakaokuwepo uwanjani. Mashabiki wa Simba wanatarajia kushuhudia burudani babukubwa huku timu yao ikipambania ushindi ambao ni muhimu katika kuendeleza mbio zao za kubeba ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, anatarajiwa kutangaza rasmi kikosi kitakachoshuka dimbani dhidi ya Yanga majira ya saa 10 jioni. Huku mashabiki na wadau wa soka wakisubiri kwa hamu kikosi hicho, hapa tumekuandalia orodha ya wachezaji tunao tarajia kuwaona wakianza katika mtanange huu kutokana na viwango walivyoonyesha kwenye michezo iliyopita.

Kikosi cha Simba Vs Yanga Leo 19/10/2024

Angalia hapa Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 19/10/2024

Kikosi hiki cha utabiri kimezingatia uwezo na michango ya wachezaji katika mechi zilizopita, na kinaweza kutoa mwanga wa nani atakuwa na nafasi ya kuongoza mashambulizi dhidi ya mahasimu wao, Yanga.

Utabiri wa Kikosi cha Simba dhidi ya Yanga leo:

  • Kipa: Camara
  • Beki wa Kulia: Shomari Kapombe
  • Beki wa Kushoto: Mohammed Hussein
  • Beki wa Kati: Abdlazack Hamza
  • Beki wa Kati: Che Malone
  • Kiungo Mkabaji: Yusuph Kagoma
  • Winga wa Kulia: Kibu Denis
  • Kiungo wa Katikati: Debora Fernandes
  • Winga wa Kushoto: Jean Ahoua
  • Kiungo Mshambuliaji: Moses Mutale
  • Straika: Leonel Ateba

Matarajio ya Simba SC

Simba, inayojulikana kwa uchezaji wake wa kasi na mbinu za kushambulia, inatazamia kudumisha rekodi yao ya kutopoteza msimu huu wa 2024/25. Katika michezo yao mitano ya ligi, wamefanikiwa kushinda michezo minne na kutoka sare mara moja.

Matokeo yao ya hivi karibuni yalikuwa sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa KMC, lakini Simba wanajivunia ushindi mkubwa wa 4-0 dhidi ya Fountain Gate na 3-0 dhidi ya Tabora United.

Hata hivyo, Simba wanakabiliwa na changamoto kadhaa za majeruhi kuelekea mchezo huu muhimu. Ayoub Lakred, mmoja wa wachezaji tegemezi wa timu, hatokuwepo kutokana na maumivu aliyoyapata wakati wa maandalizi ya msimu mpya nchini Misri.

Vilevile, Aishi Manula, kipa wao mkongwe, bado hajawa fiti kabisa, na uwezekano wa kushiriki mchezo huu ni mdogo. Pia, Abdlazack Hamza, beki aliyepata majeraha ya paja akiwa na Taifa Stars, ameanza mazoezi, lakini ushiriki wake utategemea ripoti ya madaktari.

Kwa upande mwingine, Ellie Mpanzu, ingizo jipya la Simba, bado hajakamilisha usajili wake, hivyo hawezi kucheza hadi dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa. Hata hivyo, wachezaji kama Yusuph Kagoma na Mzamiru Yassin wameanza mazoezi na kuna matumaini kwamba watakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza leo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fred Minziro Akabidhiwa Rasmi Mikoba ya Kuinoa Pamba jiji
  2. Timu Zilizofuzu AFCON 2025
  3. Taifa Stars Yashushiwa Kichapo Mbele ya Maelfu Ya Mashabiki Kwa Mkapa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo