Kikosi cha Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya TMA Kombe la Shirikisho
BAADA ya kushindwa kuchezwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo wikiendi iliyopita dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara, leo jioni Simba itashuka dimbani kuvaana na TMA Stars ya Arusha katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (FA). Mechi hii inachezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Hii ni moja kati ya mechi tatu zinazopigwa leo kwenye FA Cup, huku nyingine zikiwa ni kati ya Kiluvya United dhidi ya Pamba Jiji, na Kagera Sugar dhidi ya Namungo. Washindi wa michezo hii watasonga mbele na kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, ambayo itaanza rasmi Alhamisi. TMA Stars, inayofundishwa na kocha Mohamed Ismail ‘Laizer,’ inashika nafasi ya tano katika Ligi ya Championship. Timu hii itakabiliana na Simba inayoshika nafasi ya pili Ligi Kuu Bara, ikiwa na kikosi thabiti kinachotegemewa kuonyesha ubora wake leo jioni.
Kocha wa Simba, Faldu Davis, anategemewa kutumia kikosi imara kinachojumuisha washambuliaji mahiri kama Leonel Ateba, Jean Ahoua, na Steven Mukwala. Kwa upande mwingine, Kocha Laizer wa TMA Stars amekiri kuwa changamoto kubwa kwa timu yake ni safu ya ulinzi, ambayo imeruhusu mabao 20 katika mechi 22 za Championship msimu huu.
Katika mechi ya awali ya FA Cup hatua ya 64 Bora, Simba iliichapa Kilimanjaro Wonders mabao 6-1, huku TMA Stars nayo ikionyesha makali kwa kuichapa Leopards mabao 5-1. Hii inaashiria kwamba mashabiki wa soka wanapaswa kutarajia mchezo wa kusisimua.
Kikosi cha Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025
Kikosi rasmi cha Simba Leo kitakachoshuka dimbani kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 15:00 jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Faldu Davis atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo TMA Stars itapambana kuwashangaza mashabiki wa soka.
Takwimu Muhimu Kabla ya Mechi
- Simba imefunga mabao 46 na kuruhusu manane pekee katika Ligi Kuu msimu huu.
- TMA Stars imeruhusu mabao 20 katika mechi zake 22 za Championship.
- Washambuliaji wa Simba kama Ateba na Mukwala wanatarajiwa kuwa tishio kwa mabeki wa TMA Stars.
- TMA Stars inawategemea nyota wake kama Bastian Joseph, Abdul Aziz Shahame, na Sixtus Sabilo ili kuleta upinzani kwa Simba.
Simba inaingia katika mechi hii kama timu yenye nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora wake wa safu ya ushambuliaji na rekodi nzuri ya msimu huu. Hata hivyo, TMA Stars haipaswi kudharauliwa kwani inaweza kuleta mshangao kwa kutumia mbinu za kushambulia kwa kushtukiza.
Kikosi rasmi cha Simba kinatarajiwa kutangazwa rasmi majira ya saa 15:00 jioni. Mashabiki wanapaswa kuwa macho kusubiri orodha kamili ya wachezaji watakaoshuka dimbani. Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua, huku TMA Stars ikijipanga kutoa upinzani mkali dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa FA Cup.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba vs TMA Stars Leo 11/03/2025 Saa Ngapi?
- Yanga VS Simba Leo 08/03/2025 Saa Ngapi?
- Mechi ya Leo ya Yanga Dhidi ya Simba Yaahirishwa
- Kikosi cha Yanga Vs Simba Leo 08/03/2025
- Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Yanga 08/03/2025
- Simba Yatangaza Kususia Mechi Dhidi ya Yanga Leo 08/03/2025: Nini Chanzo?
- Tabora United Kuwakabili JKT Tanzania CCM Kirumba Machi 7, 2025
Leave a Reply