Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki

Leo, tarehe 28 Julai 2024, mashabiki wa soka watashuhudia mtanange wa kirafiki kati ya wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, na timu ya Telecom Egypt. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Mercure kuanzia saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo huu ni sehemu muhimu ya maandalizi ya klabu Simba kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kuanza tarehe 8 Agosti. Wekundu wa Msimbazi watakuwa wakijaribu wachezaji wao wapya waliosajiliwa pamoja na mbinu zao za ushindi dhidi ya Telecom Egypt kabla ya kukutana na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, kwenye mchezo wa ngao ya jamii.

Huu utakuwa mchezo wa pili wa kirafiki kwa Simba katika kipindi hiki cha maandalizi ambacho wapo katika kambi maalumu Misri. Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya El-Qanah ya Misri, Simba ilionyesha uwezo mkubwa kwa kushinda magoli 3-0. Jean Charles Ahoua alifunga magoli mawili ya haraka katika dakika za mwanzo, huku Okejepha akifunga goli la tatu na la mwisho katika dakika za nyongeza.

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kwa hamu kuona jinsi Simba itakavyocheza dhidi ya Telecom Egypt. Je, wekundu wa Msimbazi wataendeleza wimbi lao la ushindi? Au Telecom Egypt itatoa upinzani mkali? Majibu ya maswali haya yatapatikana leo usiku kwenye uwanja wa Mercure. Hapa tutakuletea kikosi rasmi cha Simba Sc Vs Telecom Egypt mara baada ya kutangazwa na kocha wa Simba.

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 - Mechi ya Kirafiki

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki

Hiki apa kikosi rasmi cha simba sc leo

  1. Hussein Abel
  2. David Kameta
  3. Valentin Nouma
  4. Hussein Kazi
  5. Abdulazak Hamza
  6. Augustine Okajepha
  7. Ladaki Chasambi
  8. Debora Fernandez
  9. Freddy Micanel
  10. Omary Omary
  11. Salen Karabaka

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 - Mechi ya Kirafiki

Kikosi Cha Utabiri: Ally Salim (1) Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15) Karaboue Chamou (2) Che malone (20) Mzamiru Yassin (19) Yusuph Kagoma (21) Edwin Balua (16) Joshua Mutale (7) Jean Charles Ahoua (10) Freddy Michael (18).

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup
  2. Kikosi Cha Yanga Vs Kaizer Chiefs 28 July 2024 – Toyota Cup
  3. Hizi Apa Picha Za Jezi Mpya Ya Yanga Sc 2024/2025
  4. Hivi Apa Vituo Vya Kununua Tiketi Simba Day 2024
  5. PSL Betway Premiership Fixtures 2024/2025
  6. Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
  7. Yanga Yapata Mserereko CAF: Mechi Zote za Klabu Bingwa Kupigwa Dar es Salaam
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo