Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 | Kikosi Cha Simba Leo Dhidi ya Tanzania Prisons
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watashuka dimbani kuvaana na Wajelajela, Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni. Ni mechi muhimu kwa timu zote mbili, zikiwa na malengo tofauti lakini yenye umuhimu mkubwa katika msimamo wa ligi.
Simba SC, inayonolewa na Kocha Fadlu Davids, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na dhamira ya kurekebisha makosa ya mechi iliyopita dhidi ya Fountain Gate, ambapo walilazimishwa sare ya 1-1 ugenini. Matokeo hayo yaliharibu rekodi nzuri ya ushindi mfululizo ugenini, hivyo leo watahitaji ushindi ili kuendelea kupambana kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Yanga.
Kwa mujibu wa takwimu, Simba SC imepoteza mechi moja tu kati ya nane zilizopita nyumbani, huku ikipata sare moja. Kwa hivyo, ushindi leo utakuwa muhimu ili kurejesha rekodi nzuri ya nyumbani.
Kwa upande wa Tanzania Prisons, kikosi hiki kimeanza duru la pili kwa kasi, kikishinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Pamba Jiji (1-0) na Mashujaa (2-1). Maafande hao wa Magereza wanashika nafasi ya tatu kutoka chini kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 17 baada ya michezo 17. Hii inamaanisha kuwa wanahitaji ushindi ili kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.
Tanzania Prisons hivi sasa inafundishwa na Kocha Amani Josiah, aliyerithi mikoba ya Mbwana Makata aliyesitishiwa mkataba wake Desemba 28, 2024. Josiah ameeleza kuwa anawaambia wachezaji wake wasiwe na presha kwani ni kawaida kwa timu kama Prisons kufungwa na timu kubwa kama Simba, Yanga na Azam FC. Hata hivyo, anasema kuwa kikosi chake hakina majeruhi, hali inayowapa nafasi nzuri ya kupambana na Simba SC.
Kikosi cha Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya Tanzania Prisons kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Rekodi za Hivi Karibuni na Historia ya Mikutano yao
Katika mechi 10 za mwisho kati ya timu hizi mbili, Simba SC imeshinda mara tano, Tanzania Prisons ikishinda mara tatu, huku michezo miwili ikimalizika kwa sare. Hata hivyo, mechi nyingi kati ya hizi zimekuwa na idadi ndogo ya mabao, isipokuwa ile ya Desemba 30, 2022, ambapo Simba SC iliichapa Prisons mabao 7-1.
Katika duru la kwanza la msimu huu, Simba SC iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons. Lakini kutokana na mabadiliko ya kiufundi kwenye kikosi cha Prisons, pamoja na ari mpya waliyo nayo, mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mgumu na wa ushindani mkubwa.
Mikakati ya Makocha
Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa wamejipanga kutumia mbinu za kushambulia kwa kasi ili kupata mabao ya mapema. Anaamini kuwa kufunga mapema kunawavuruga wapinzani na kuwafanya kupoteza kujiamini, hivyo watatumia mfumo huo leo dhidi ya Tanzania Prisons.
Kwa upande wake, Kocha Josiah wa Prisons anajua kuwa hawawezi kumiliki mpira kwa uwiano wa 50/50 dhidi ya Simba SC. Hata hivyo, anaamini kuwa kikosi chake kina uwezo wa kuhimili presha na kushambulia kwa tahadhari kubwa. Amewataka wachezaji wake kufurahia mchezo bila kuhisi presha kubwa ya lazima kushinda.
Wachezaji wa Kufuatilia
Kwa Simba SC, macho yote yatakuwa kwa wachezaji wake wa safu ya ushambuliaji, ambao wamekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha wanapata mabao ya mapema. Pia, bado kuna maswali kuhusu hali ya Kibu Denis, ambaye yupo chini ya uangalizi wa kitabibu na bado haijathibitishwa kama atacheza.
Kwa Tanzania Prisons, wachezaji walioweka rekodi nzuri kwenye mechi mbili zilizopita watajaribu kuendeleza kiwango chao bora, hasa kwa kuzingatia kuwa wanaingia kwenye mchezo huu bila majeruhi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?
- YANGA warejea nyumbani na pointi moja baada ya sare na JKT Tanzania
- Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
- Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
- Ratiba ya Mechi za Leo 10 Februari 2025
- Viingilio Mechi ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
- JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025 Saa Ngapi?
- Bao la Kaseke Laipa Pamba Ushindi Dhidi ya Azam FC
- Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji Wampa Jeuri Minziro
- Ngassa: Mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini tunajua pakupenya
Leave a Reply