Kikosi cha Simba vs Singida BS Leo 28/12/2024 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Singida BS Ligi Kuu
Leo Saa 10:00 jioni, Singida BS watakuwa nyumbani katika Uwanja wa CCM Liti wakiwakaribisha wekundu wa msimbazi Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ya Tanzania Bara. Singida BS wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, huku Simba SC wakiwa wanaongoza msimamo wa ligi. Mechi hii itarushwa moja kwa moja kupitia chaneli ya AzamSports1HD katika kisimbuzi cha Azam, ikiwa ni moja ya michezo miwili ya ligi inayotarajiwa kufuatiliwa kwa ukaribu leo.
Simba SC wameonyesha ubora mkubwa msimu huu, wakiwa hawajapoteza mechi yoyote kati ya nane zilizopita tangu kufungwa na Yanga mnamo Oktoba 19, 2024. Katika mechi hizo nane, Simba wamefunga mabao 17 na kuruhusu mawili pekee. Kocha Fadlu Davids anatarajia timu yake itamaliza duru la kwanza ikiwa kileleni kwa pointi 40, huku ushindi wa leo ukiwa muhimu sana kwa mafanikio yao ya msimu huu.
Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na pointi 37, moja zaidi ya Yanga walio nafasi ya pili. Kwa ushindi wa leo, Simba wataendelea kuimarisha nafasi yao kileleni, lakini matokeo tofauti yanaweza kuwaweka katika presha kubwa ikiwa Yanga watashinda mchezo wao kesho.
Singida BS, licha ya kuwa nafasi ya nne kwa pointi 33, wameonyesha mwelekeo mzuri msimu huu. Timu hii ina wachezaji nyota kama Elvis Rupia, kinara wa mabao katika ligi akiwa amefunga mara nane. Katika mchezo wao uliopita, walishinda dhidi ya KenGold kwa mabao 2-1. Kocha wa Singida BS, Sead Ramovic, anatarajia kikosi chake kitatoa ushindani mkubwa dhidi ya Simba, huku wakilenga kuvunja rekodi mbaya dhidi ya wapinzani wao hao.
Hadi sasa, Singida BS wamekutana na Simba mara saba, wakipoteza michezo sita na kutoka sare moja. Hata hivyo, ubora wa kikosi chao msimu huu unawapa matumaini ya matokeo chanya.
Kikosi cha Simba vs Singida BS Leo 28/12/2024
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya Singida BS kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Wachezaji wa Kuzingatia
Katika safu ya ushambuliaji, Simba wanamtegemea Jean Charles Ahoua aliyefunga mabao saba na kutoa asisti 11 msimu huu, pamoja na Leonel Ateba mwenye mabao matano. Steven Mukwala pia anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi zilizopita.
Kwa upande wa Singida BS, Elvis Rupia anaongoza safu yao ya ushambuliaji, akisaidiwa na wachezaji kama Marouf Tchakei na Victorien Adebayor. Aidha, kipa wao Metacha Mnata, mwenye clean sheet saba msimu huu, anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi.
Matarajio ya Mechi
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, ukiwaleta pamoja timu mbili zenye wachezaji wa kimataifa na wazawa wenye uwezo wa hali ya juu. Simba wanatazamiwa kutumia uzoefu wao wa michezo mikubwa, huku Singida BS wakilenga kuendeleza kiwango chao bora msimu huu.
Katika mechi tano zilizopita, Simba wameshinda zote, huku Singida BS wakishinda tatu, sare moja, na kupoteza moja. Ushindi wa leo kwa timu yoyote utakuwa muhimu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Mashabiki wanatarajia burudani ya kiwango cha juu na ushindani wa kweli kutoka kwa timu zote mbili. Je, Simba wataendeleza rekodi yao nzuri, au Singida BS wataweka historia kwa kuibuka na ushindi? Tusubiri kuona matokeo!
Mapendekezo ya Mhariri:
- Singida Bs VS Simba Sc Leo 28/12/224 Saa Ngapi?
- Penati ya Dakika za Majeruhi Yaipa Simba Pointi Tatu Dhidi ya JKT
- Shaban Chilunda Awindwa na KMC
- Yanga Yaibuka na Pointi tatu Dhidi ya Tanzania Prisons
- Vita ya Kumsajili Okoyo Yazuka Kati ya KMC, Mashujaa na Namungo
- Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2024/2025
Leave a Reply