Kikosi cha Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024 | Kikosi cha Simba leo Dhidi ya JKT Tanzania
Kikosi cha Simba leo kitakuwa dimbani kuwakabili wageni wao JKT Tanzania katika mchezo wa NBC Premier League, ambao umepangwa kuanza saa 10:15 jioni katika uwanja wa KMC Complex, Mwenge. Mchezo huu ni wa kiporo baada ya JKT Tanzania kukumbwa na ajali walipokuwa wakirejea Dar es Salaam kutoka Dodoma.
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, ameweka wazi kuwa Wekundu wa Msimbazi wanaingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu—kusaka ushindi wa kujiimarisha katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi. Matola amesema Simba itabadilika kiuchezaji kulingana na mbinu za mpinzani wao, ili kuhakikisha kuwa wanawachanganya JKT Tanzania na kuzuia maandalizi ya wapinzani hao kufanikisha lengo lao.
“Tutaingia na mpango mkakati wetu, lakini tutabadilika kulingana na namna wao wanavyobadilika. Tunataka kuhakikisha wanakutana na hali tofauti na walichokizoea mazoezini,” alisema Matola.
Pia, alisisitiza kuwa mechi haitakuwa rahisi kwani JKT Tanzania ni miongoni mwa timu zinazocheza vizuri licha ya kutopata matokeo bora hivi karibuni. Wachezaji wa Simba wameshughulikia changamoto ya kuruhusu mabao mepesi, ambayo imekuwa ikiwakosesha furaha benchi la ufundi.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Ahmad Ally, ameisifia Simba kwa kiwango chao cha juu, hasa baada ya Kocha Fadlu Davids kuunda kikosi imara chenye mawinga wenye kasi na mfumo wa kushambulia muda mwingi. Ally alisema wamejiandaa kukabiliana na changamoto za Simba, hasa katika mipira ya kona na faulo, ambavyo ni hatari kubwa kwa wapinzani wao.
“Timu bora lazima ikutane na timu bora nyingine. Tumejipanga kucheza vizuri iwe tuna mpira au hatuna, na kuhakikisha tunakuwa wa kwanza katika kila tukio uwanjani,” alisema kocha huyo.
Hata hivyo, JKT Tanzania ina changamoto ya kutokushinda wala kufunga bao katika michezo mitatu mfululizo ya ligi, jambo linalowapa presha ya kuhakikisha wanapata matokeo chanya dhidi ya Simba.
Kikosi cha Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya JKT Tanzania kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Changamoto na Upekee wa Mechi Hii
Mechi hii ni ya kipekee kwa sababu inazikutanisha timu mbili zenye malengo tofauti. Simba wanapigania kuimarisha nafasi zao za juu, huku JKT Tanzania wakisaka ushindi wa kwanza baada ya kipindi kigumu. Kwa upande wa Simba, mfumo wa kubadilika kulingana na hali ya mchezo unaweza kuwapa faida, lakini pia utahitajika umakini mkubwa ili wasifanye makosa.
Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, ukichochewa na ubora wa kikosi cha Simba na ari ya JKT Tanzania ya kurejea kwenye ushindi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply