Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya Fountain Gate
Baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga SC, kuwashushia kichapo cha mabao 6-1 Kengold na kufanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, leo ni zamu ya Simba SC kuingia dimbani dhidi ya Fountain Gate FC kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati. Mchezo huu ni muhimu kwa Wekundu wa Msimbazi kwani ushindi utawarejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Simba SC inaendelea na maandalizi ya mechi hii huku ikiwa na wasiwasi juu ya uwepo wa mshambuliaji wake tegemeo, Kibu Denis. Kibu aliumia katika mechi yao iliyopita dhidi ya Tabora United, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora. Katika mchezo huo, nafasi yake ilichukuliwa na Ladack Chasambi.
Daktari wa Simba, Edwin Kagabo, amesema kuwa Kibu anaendelea na matibabu na uwezekano wa kucheza dhidi ya Fountain Gate uko hamsini kwa hamsini.
“Mchezaji wetu alipata changamoto katika sehemu mbili kwenye mchezo wetu dhidi ya Tabora United. Alipata shida kwenye enka na pia kwenye sehemu ya robo tatu ya chini ya mguu. Kwa hivyo hali yake hadi sasa hivi iko vizuri na anaendelea na matibabu,” alisema Kagabo.
Hata hivyo, Kagabo aliwahakikishia mashabiki wa Simba kuwa hali ya mchezaji huyo si mbaya sana, lakini uamuzi wa mwisho kuhusu ushiriki wake katika mechi dhidi ya Fountain Gate utafanywa baada ya tathmini ya mwisho.
Kwa upande mwingine, wachezaji wengine 23 wa kikosi cha Simba wako katika hali nzuri na wanajiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huu muhimu. Mchezo huu ni wa muhimu kwa Simba SC kwani ushindi utaiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Mashabiki wa Simba wanatarajia kuona timu yao ikipambana vikali kuhakikisha inapata alama tatu muhimu dhidi ya Fountain Gate FC.
Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya Fountain Gate kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tisa alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Muda na Mahali pa Mchezo
Mchezo huu wa Fountain Gate vs Simba SC utapigwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, na utachezwa Alhamisi, Februari 6, 2025, kuanzia saa 10:15 jioni. Mashabiki wa soka Tanzania wanatarajia pambano kali, huku Simba ikisaka ushindi wa kuendelea kuongoza ligi, wakati Fountain Gate nayo ikihitaji matokeo mazuri ili kujiondoa kwenye nafasi za chini za msimamo. Je, Simba itaweza kurejea kileleni mwa ligi? Tusubiri kuona.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Fountain Gate VS Simba Leo 06 Februari 2025 Saa Ngapi?
- RATIBA ya Mechi za Leo 06 Februari 2025
- CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
- Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
- Kilichomuondoa Ramovic Yanga Hatimaye Chafichuka
- CAF Yatangaza Tarehe ya Droo Robo Fainali ya Klabu Bingwa na Shirikisho
- Kikosi cha Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
- Ratiba ya Mechi za Leo 05/02/2025
Leave a Reply