Kikosi cha Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya CS Sfaxien
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo wataikaribisha CS Sfaxien ya Tunisia katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Uwanja huu, unaojulikana kama “machinjio ya mnyama,” umekuwa ngome ya ushindi kwa klabu ya Simba, hasa katika mashindano ya kimataifa.
Mchezo huu wa Kombe la Shirikisho Afrika unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku mashabiki wakitegemea ushindi wa nyumbani ili kuimarisha nafasi ya Simba katika hatua ya makundi.
Simba na CS Sfaxien zinakutana kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano ya CAF.
Hata hivyo, timu zote zina rekodi nzuri kwenye mashindano ya Afrika. CS Sfaxien, mabingwa wa Kombe la Shirikisho mara tatu (2007, 2008, 2013), wapo katika presha kubwa baada ya kupoteza mechi zao mbili za awali kwenye hatua ya makundi. Kwa upande mwingine, Simba inashika nafasi ya pili kwenye Kundi A, ikiwa na alama tatu baada ya ushindi dhidi ya Bravos do Maquis kutoka Angola.
Katika mechi zao tano za hivi karibuni, Simba imeonyesha uimara mkubwa, ikishinda mechi nne na kupoteza moja pekee. Kwa upande wa CS Sfaxien, wamekuwa wakisuasua, wakiwa na ushindi mara mbili pekee kwenye Ligi ya Tunisia na kupoteza mechi zao mbili za CAF.
Kocha wa Simba, Fadlu David, amesisitiza umuhimu wa ushindi katika mchezo huu. Akizungumza kabla ya mechi, alisema:
“Tunahitaji pointi tatu. Tumekuwa na maandalizi mazuri na mabadiliko ya kimbinu yatasaidia kuimarisha kikosi. Nawaomba Wanasimba wajitokeze kwa wingi kutusapoti. Kwa pamoja tunaweza. Simba nguvu moja!”
Fadlu anapendelea kutumia mfumo wa kisasa wa 4-2-3-1, ambao umewawezesha Wekundu wa Msimbazi kudhibiti mchezo na kushambulia kwa ufanisi. Mfumo huu unategemea viungo wa kati kama Fabrice Ngoma na Augustine Okejepha kwa kudhibiti uwanja wa kati, huku washambuliaji wa pembeni kama Kibu Denis na Edwin Balua wakipewa nafasi ya kuvuruga ngome ya CS Sfaxien.
Katika eneo la ulinzi, mabeki Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, na Fondoh Che Malone watalinda lango la kipa Moussa Camara, ambaye amekuwa na kiwango kizuri kwenye michuano ya CAF.
Kikosi cha Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya CS Sfaxien kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa tatu usiku. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Changamoto kwa Simba
Licha ya kuwa na rekodi nzuri ya nyumbani, Simba inakabiliwa na changamoto katika safu ya ushambuliaji. Kutokuwa na umakini kwenye eneo hili kumeigharimu timu mabao muhimu katika mechi zilizopita, ambapo goli la penalti dhidi ya Bravos lilikuwa tegemeo pekee la ushindi. Kocha Fadlu anatarajiwa kurekebisha hali hii kwa kuhakikisha washambuliaji wanakuwa na utulivu wa kutosha mbele ya goli.
CS Sfaxien: Kikosi na Mbinu
CS Sfaxien, licha ya kuwa na historia tajiri, wanakabiliwa na changamoto kubwa msimu huu. Safu yao ya ulinzi imeonekana dhaifu, ikiruhusu mabao mengi katika mechi za hivi karibuni. Hata hivyo, wanatarajiwa kuja na mbinu mpya wakilenga kusaka ushindi wao wa kwanza kwenye hatua ya makundi.
Wachezaji muhimu wa CS Sfaxien ni pamoja na viungo wao mahiri, ambao wanatarajiwa kutoa ushindani mkali kwa viungo wa Simba. Licha ya changamoto zao, Sfaxien bado ni timu yenye uzoefu mkubwa na hawatakuwa wapinzani wa kubezwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024 Saa Ngapi?
- Jackson Shiga Anukia Fountain Gate
- Bao la Mwisho la Dube Laipa Yanga Point dhidi ya TP Mazembe
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024
- Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024
- Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?
Leave a Reply