Kikosi cha Simba VS Bravos do Maquis Leo 12/01/2025 | Kikosi cha Simba leo Dhidi ya Bravos do Maquis CAF
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo saa 1:00 usiku watakuwa na kibarua kizito kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Mechi hii muhimu itapigwa katika Uwanja wa 11 de Novembro, Luanda, Angola, ambapo Simba watakutana na Bravos do Maquis katika raundi ya tano ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF. Ushindi au sare kwa Simba leo unatosha kuwahakikishia nafasi ya kusonga mbele kutoka Kundi A.
Simba na Bravos tayari zimekutana mara moja msimu huu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam, ambapo Simba walishinda 1-0 kwa penalti ya Jean Charles Ahoua dakika ya 27. Simba sasa wanashika nafasi ya pili kwenye kundi wakiwa na alama tisa, sawa na CS Constantine wanaoongoza kwa tofauti ya mabao. Kwa upande wa Bravos, wanashika nafasi ya tatu na alama sita, huku CS Sfaxien wakiwa hawana alama baada ya kupoteza michezo yote minne.
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa mchezo wa leo una umuhimu mkubwa si kwa Simba pekee bali pia kwa wapinzani wao. Simba wanahitaji kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili kupunguza presha ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Constantine Januari 19 jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Davids, kikosi cha Simba kimejiandaa vizuri licha ya changamoto za muda mfupi wa mapumziko kati ya mechi.
“Umuhimu wa mchezo huu ni mkubwa kwa timu yetu. Tumepata mapokezi mazuri Angola, hali ya hewa ni rafiki, na tunajua malengo yetu ni kupambana na kupata ushindi,” alisema Davids.
Simba imeonyesha uwezo mkubwa msimu huu, hasa katika kipindi cha kwanza cha mechi zao. Mabao sita kati ya nane waliyoifunga kutoka hatua ya mtoano hadi sasa yamepatikana kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa eneo la kiungo, akiwemo Jean Charles Ahoua na Kibu Denis, wamekuwa chachu ya ushindi wa timu. Kikosi kilichoenda Angola kimejumuisha viungo 11 kati ya wachezaji 22, jambo linaloonyesha mkakati wa timu kutawala mchezo katikati ya uwanja.
Kwa upande wa Bravos, wanajivunia rekodi yao ya kutofungwa nyumbani msimu huu kwenye michuano ya CAF, wakiwa wameshinda mechi zote nane. Wachezaji wao hatari ni Jo Paciencia na Francisco Cabuema “Macaiabo,” ambao kila mmoja amefunga mabao matatu msimu huu. Timu hii pia inajulikana kwa kutumia vyema kipindi cha kwanza, ambapo mabao saba kati ya 12 waliyofunga msimu huu yametokana na dakika za mwanzo.
Kikosi cha Simba VS Bravos do Maquis Leo 12/01/2025
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya Bravos kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025
- Kikosi cha Yanga VS Al Hilal Leo 12/01/2025
- Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Leo 12/01/2025
- Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025 Saa Ngapi?
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
- AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
- Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
Leave a Reply