Kikosi cha Simba vs Al Ahly Tripoli Leo – Kombe la Shirikisho AFrika CAF | Hiki Apa Kikosi Cha Simba Leo Vs Al Ahly Tripoli ya Libya CAF Confederation Cup
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, ametangaza rasmi kikosi kitakachoanza katika mchezo wa hatua za awali za Kombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya Al Ahly Tripoli kutoka Libya. Mchezo huu utaanza kutimua vumbi rasmi majira ya saa mbili kamili usiku katika Uwanja wa Tripoli INT, Tripoli, Libya, na utarushwa moja kwa moja kupitia king’amuzi cha Azam TV.
Simba SC wanakutana na Al Ahly Tripoli wakiwa na lengo moja kubwa la kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea mechi ya marudiano itakayochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ushindi au sare katika mechi hii itawapa faida kubwa Simba katika kuhakikisha wanaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa tano mfululizo.
Hiki Apa Kikosi cha Simba vs Al Ahly Tripoli Leo – Kombe la Shirikisho AFrika
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, amefanya mabadiliko katika kikosi chake kwa mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly Tripoli katika hatua za awali za Kombe la Shirikisho Afrika CAF. Hiki hapa ni kikosi kamili kitakachoanza uwanjani leo:
Kikosi Cha Simba SC:
- 40 Camara – Kipa
- 12 Kapombe – Beki wa kulia
- 15 Hussein – Beki wa kushoto
- 14 Hamza – Beki wa kati
- 20 Che Malone – Mlinzi wa Kati
- 21 Kagoma – Kiungo
- 37 Balua – Kiungo
- 17 Fernandes – Kiungo
- 13 Ateba – Mshambuliaji
- 10 Ahoua – Kiungo Mshambuliaji
- 26 Mutale – Mshambuliaji
Wachezaji wa Akiba (Subs): Ally, Kujili, Chamou, Ngoma, Okejapha, Kibu, Awesu, Mkwala & Mashaka
Takwimu na Uchambuzi wa Mechi
Simba imeonyesha uimara wa kitimu katika mechi za kimashindano zilizopita, ikifanikiwa kucheza mechi nne bila kuruhusu mabao mengi. Katika mechi hizo nne, Simba imeruhusu bao moja pekee, jambo linaloashiria uimara wa safu ya ulinzi.
Hii ni wastani wa bao 0.3 kwa kila mchezo, huku Simba wakifunga mabao nane, ambayo ni wastani wa mabao mawili kwa kila mechi.
Kwa upande wa wapinzani wao, Al Ahly Tripoli wameonyesha udhaifu mkubwa katika safu ya ulinzi. Katika mechi 10 zilizopita, timu hiyo ya Libya imeruhusu nyavu zao kutikiswa mara 10, ikiwa ni wastani wa bao moja kwa kila mchezo.
Udhaifu huu unatoa mwanya kwa Simba kutumia nafasi zozote wanazopata kujaribu kufunga mapema.
Hata hivyo, Al Ahly Tripoli inategemewa kuja na safu ya ushambuliaji yenye nguvu, ikiongozwa na mshambuliaji hatari, Agostinho Cristóvão Paciência, maarufu kama Mabululu.
Katika mechi zake 10 zilizopita, Al Ahly imefunga mabao 16, ikiwa ni wastani wa bao 1.6 kwa kila mchezo. Rekodi yao ya ushindi nyumbani pia ni ya kuvutia, wakiwa wameshinda mechi saba kati ya 10 walizocheza nyumbani katika mashindano ya kimataifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply