Kikosi cha Simba SC vs Stellenbosch Leo 27 April 2025 | Kikosi cha Simba Kinachoanza Leo Dhidi ya Stellenbosch | Kikosi cha Kwanza Cha Simba Dhidi ya Stellenbosch Nusu Fainali Shirikisho CAF
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo tarehe 27 Aprili 2025 watashuka dimbani kuivaa timu ya Stellenbosch FC katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025. Mchezo huu muhimu utatimua vumbi katika Uwanja wa Moses Mabhida, Durban, Afrika Kusini kuanzia saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Mchuano huu una umuhimu mkubwa kwani ndio utakaoamua timu ipi itatinga katika fainali za michuano hiyo, huku Simba wakiwa na faida ya ushindi wa goli moja walioupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Katika mchezo wa kwanza, Simba SC walifanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 lililofungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 45+2 kupitia mpira wa adhabu. Ushindi huo unawaweka katika nafasi nzuri, hata hivyo, masharti ya mchezo wa leo yanawataka kuwa makini zaidi ili kuhakikisha wanaendeleza mafanikio hayo na kufuzu bila kusubiri hatua ya mikwaju ya penalti, endapo Stellenbosch watapata bao la kusawazisha.
Kikosi cha Simba SC vs Stellenbosch Leo 27 April 2025
Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 09:00 jioni. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Faldu Davis atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo Stellenbosch itakua na jukumu la kuonesha ubabe wake nyumbani, huku Simba ikipambana kuulinda ubingwa wao wa goli moja walioupata wakiwa nyumbani.
Fuatilia Pia: Matokeo ya Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025
Kikosi kinachotarajiwa kuanza kwa Stellenbosch ni:
Sage Stephens, Enyinnaya Godswill, Fawaaz Basadien, Thabo Moloisane, Ismael Olivier Touré, Genino Palace, Sihle Nduli, Thato Khiba, Devin Titus, Lesiba Nku, na Andre de Jong.
Kwa upande wa Simba SC, Chamou Karaboue ambaye alikuwa majeruhi katika mchezo wa awali, sasa afya yake imeimarika na anatarajiwa kuwepo kikosini. Hakuna taarifa ya mchezaji mwingine yeyote kukosekana kutoka kikosi kilichocheza mechi ya kwanza.
Kikosi kinachotarajiwa kuanza kwa Simba SC ni:
Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Chamou Karaboue, Fabrice Ngoma, Yusuph Kagoma, Kibu Denis, Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu, na Steven Mukwala.
Mbinu na Maandalizi ya Makocha
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ameeleza wazi kuwa lengo la timu yake katika mchezo wa leo si tu kulinda ushindi wa nyumbani bali pia kushambulia ili kupata bao la mapema. Kwa mujibu wa Davids, dakika kumi za kwanza zitakuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua mwelekeo wa mechi, akisisitiza kuwa Simba haitacheza kwa kujilinda wala kwa woga. Kauli yake inaonyesha dhamira ya timu kuingia uwanjani kwa nguvu kamili, kujaribu kumaliza mchezo mapema kwa kupata bao la kuwachanganya wapinzani wao.
Aidha, Davids alifafanua kuwa maandalizi ya kikosi chake yamekuwa makini, si kwa ajili ya nusu fainali pekee, bali kwa lengo la kutwaa ubingwa wa mashindano haya. Alisisitiza kuwa ingawa sare ingeweza kuwatosha kufuzu, msimamo wa Simba ni kupigania ushindi katika kila mchezo.
Kwa upande mwingine, kocha wa Stellenbosch, Steve Barker, amebainisha kuwa pamoja na kushindwa katika mchezo wa kwanza, anayo imani kubwa kuwa kikosi chake kina uwezo wa kupindua matokeo.
Barker alieleza kuwa kiwango walichoonesha Zanzibar kinawapa matumaini makubwa, na akasisitiza kuwa wataingia kwa ari ya kushambulia kutafuta bao la mapema ili kusawazisha na kuendeleza matumaini ya kufika fainali.
Kwa kuzingatia maelezo ya makocha wote wawili, matarajio ni kwamba dakika 45 za kwanza zitakuwa na kasi kubwa, kila timu ikitafuta bao la kuamua mwelekeo wa mchezo.
Wachezaji wa Kuangaliwa Katika Mechi hii
Mchezaji wa Simba SC, Jean Charles Ahoua, ameonesha kuwa ni tegemeo kubwa msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho. Hadi sasa, Ahoua amefunga mabao matatu katika mashindano haya, yote yakiwa ya ushindi wa 1-0 kwa timu yake. Mwelekeo wake wa kufunga kipindi cha kwanza umechangia Simba kuwa na matokeo mazuri. Katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Ahoua pia ameonesha uwezo wa hali ya juu kwa kufunga mabao 12, huku mara nyingi akihakikisha Simba hauruhusu bao lolote katika mechi ambazo amefunga. Mchango wake unaonekana kuwa wa kipekee, jambo ambalo linatarajiwa kuwa muhimu katika mchezo wa leo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?
- Dickson Ambundo Ajiondoa Fountain Gate Akidai Kutolipwa Zaidi ya Shilingi Milioni 50
- Viingilio Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba VS Stellenbosch 20/04/2025
- Kikosi cha Stellenbosch Chawasili Zanzibar kwa Ajili ya Simba
- Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
- Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
Leave a Reply