Kikosi cha Simba SC vs CS Sfaxien Leo 05/01/2024 | Kikosi cha Simba Leo Dhidi ya CS Sfaxien Kombe la Shirikisho
Baada ya watani wao wa jadi, Yanga SC, kuhitimisha mpambano wao dhidi ya TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa Afrika hapo jana, leo Jumapili macho yote yanaelekezwa kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ambayo inakutana na CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ushindi katika mchezo huu unaweza kuwaweka Simba SC hatua kubwa mbele kuelekea robo fainali, huku wakihitaji pointi tatu ili kufanikisha ndoto yao ya kuingia katika hatua hiyo kwa mara ya sita ndani ya misimu saba.
Simba SC, wakiwa na pointi sita baada ya michezo mitatu, wanatarajiwa kupambana vikali kwenye Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi jijini Tunis. Timu hii inatambua kuwa rekodi zao za ugenini hazijawa za kuridhisha katika msimu huu, baada ya kutoka sare dhidi ya Al Ahli Tripoli nchini Libya na kupoteza dhidi ya CS Constantine nchini Algeria. Katika mechi kumi za hivi karibuni za kimataifa wakiwa ugenini, Simba haijapata ushindi wowote, jambo ambalo linawahamasisha wachezaji na benchi la ufundi kuondoa rekodi hiyo mbaya leo.
Kiungo wa Simba SC, Mzamiru Yassin, alibainisha umuhimu wa mchezo huu akisema, “Hatuwezi kusubiri mechi ya mwisho kuamua hatma yetu. Lazima tupambane leo ili tuwe kwenye nafasi nzuri mapema.”
Mchezo wa leo ni wa pili kwa timu hizi kukutana katika hatua hii ya makundi. Katika mchezo wa kwanza, Simba SC walifanikiwa kushinda 2-1 wakiwa nyumbani, ushindi uliopatikana kupitia juhudi za dakika za nyongeza. CS Sfaxien walionyesha uwezo wa kupambana kwa kufunga bao mapema kupitia Hazem Haj Hassen, kabla ya Kibu Denis kuleta mabao mawili ya kichwa, mojawapo likiwa la dakika ya 90+8.
Hata hivyo, Simba SC wanapaswa kuwa makini kwani CS Sfaxien, licha ya kuwa vibonde wa kundi bila pointi yoyote, wamekuwa wakionesha ushindani mkali katika kila mchezo.
Kikosi cha Simba SC vs CS Sfaxien Leo 05/01/2024
Kikosi rasmi cha Simba Sc kitakacho anza leo dhidi ya CS Sfaxien kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Simba Fadlu David.
Faida na Changamoto za Pande Mbili
Kwa upande wa Simba SC, wanakwenda katika mchezo huu wakiwa na hali nzuri. Kutokuwepo kwa mashabiki wa CS Sfaxien kutokana na adhabu waliyopewa ni pigo kwa wenyeji, jambo linalowapa Simba SC fursa ya kucheza bila shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa nyumbani. Aidha, ujio wa winga Elie Mpanzu umeongeza chaguo kwenye safu ya ushambuliaji ya kocha Fadlu Davids.
Kwa upande mwingine, CS Sfaxien wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na kocha mpya, Saad Al Daredi, ambaye amepewa timu baada ya matokeo mabaya yaliyopelekea kufutwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Alexandre Miguel Crispim Santos. Hali hii inaweza kuwa changamoto kwa wenyeji kwani mabadiliko ya benchi la ufundi mara nyingi huchukua muda kuleta matokeo mazuri.
Matarajio ya Mchezo wa Leo
Simba SC wanahitaji ushindi leo ili kufikisha pointi tisa na kuweka nafasi nzuri kuelekea robo fainali. Kwa upande wa CS Sfaxien, ushindi wao wa leo utakuwa ni wa kwanza katika kundi hili, lakini hautabadilisha nafasi yao ya mkiani, ingawa unaweza kuwapa matumaini ya kupambana katika michezo inayofuata.
Kwa kuhitimisha, mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku kila upande ukijizatiti kupata matokeo bora. Mashabiki wa soka Afrika wanasubiri kwa hamu kuona nani ataibuka mshindi katika pambano hili la kusisimua.
Mapendekezo ya Mhariri:
- CS Sfaxien vs Simba SC Leo 05/01/2024 Saa Ngapi?
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024
- Yanga Kuwakosa Maxi, Chama na Yao Mechi Dhidi ya TP Mazembe Leo
- Yanga vs Tp Mazembe Leo 04/01/2024 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Kilimanjaro Stars VS Zanzibar Heroes leo 03/01/2024
Leave a Reply