Kikosi Cha Simba kilichosafiri kwenda misri kucheza dhidi ya Al Masry
Klabu ya Simba SC kutoka Tanzania imeanza safari yake alfajiri ya jana tarehe 28 machi kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao muhimu wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAFCC) dhidi ya Al Masry. Mchezo huu wa kwanza utachezwa tarehe 2 Aprili 2025, huku marudiano yakitarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam mnamo Aprili 9, 2025.
Timu hiyo imeondoka ikiwa na kikosi chenye wachezaji 22 walioteuliwa na benchi la ufundi kwa ajili ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye uwanja wa ugenini kabla ya kurudiana nyumbani. Hapa tumekuletea orodha kamili ya wachezaji waliopo kwenye safari hiyo.
Kikosi Cha Simba SC Kilichosafiri kwenda Misri
Makipa (Goalkeepers):
- Moussa Camara
- Ally Salim
- Hussein Abel
Mabeki (Defenders):
- Karaboue Chamdou
- Abourazak Hamza
- Mohamed Hussein
- Shomari Kapombe
- Valentine Nouma
- David Kameta
- Kelvin Kijili
Viungo (Midfielders):
- Yusuph Kagoma
- Fabrice Ngoma
- Elie Mpanzu
- Debora Fernandes
- Ladack Chasambi
- Kibu Denis
- Awesu Awesu
- Jean Charles Ahoua
- Augustine Okejpha
- Joshua Mutale
Washambuliaji (Strikers):
- Leonel Ateba
- Steven Mukwala
Kwa ujumla, Simba SC imesafiri na kikosi chenye wachezaji 22, ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo wa kwanza wa robo fainali.
Wachezaji Walioachwa Nyumbani
Baadhi ya wachezaji hawakusafiri na timu na wataendelea na programu za mazoezi nyumbani. Wachezaji hao ni:
- Aish Manula
- Che Malone
- Omary Omary
- Valentine Mashaka
- Edwin Balua
- Mzamiru Yassin
Safari ya Simba SC kuelekea Misri ni hatua muhimu katika kampeni yao ya kuvunja mwiko wa kuishia robo fainali katika michuano ya ya Kombe la Shirikisho la CAF. Mashabiki wa Simba wanatarajia kuona kikosi hiki kikitoa ushindani mkali dhidi ya Al Masry katika mchezo wa kwanza, kabla ya kurudiana jijini Dar es Salaam. Je, Simba itaweza kupata matokeo chanya katika uwanja wa ugenini? Tusubiri kuona.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025
- Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025
- Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025 Saa Ngapi?
- Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035
- Aishi Manula Bado Mambo Magumu Msimbazi
- Kane Atazamia Kufikia Rekodi ya Shilton na Kuweka Historia Mpya Uingereza
- Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Kabudi na TFF, TPLB, Yanga na Simba
- CAF Yaondoa Marufuku Uwanja wa Benjamin Mkapa
- Sowah Aweka Bayana Nia Yake Yakubeba Kiatu Cha Dhahabu
- Majeraha ya Goti Yamkosesha Alphonso Davies Mechi za Mwisho za Msimu
Leave a Reply