Kikosi Cha Kilimanjaro Stars Kitakacho Shiriki Mapinduzi Cup 2025

kikosi cha kilimanjaro star

Kikosi Cha Kilimanjaro Stars Kitakacho Shiriki Mapinduzi Cup 2025

Rasmi Kikosi cha Kilimanjaro Stars kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya Kombe la Mapinduzi 2025 kimetangazwa, huku kukiwa hakuna mchezaji yeyote wa Yanga wala Simba katika kikosi hicho kwa sababu wanajiandaa na michuano ya CAF. Hii ni hatua muhimu kwa timu ya taifa ya Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuonyesha ushindani mkubwa kwenye mashindano hayo.

Maandalizi ya Mapinduzi Cup 2025

Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa 2025 itapambwa na burudani ya soka kutoka kwa timu za taifa za wakubwa. Mashindano haya yataanza rasmi tarehe 3 Januari 2025 hadi 13 Januari 2025 katika viwanja vya Gombani, Pemba. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Dkt. Suleiman Mahmoud Jabir, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup 2025, ametangaza kuwa mashindano ya mwaka huu yatahusisha timu za taifa badala ya klabu kama ilivyozoeleka.

Timu zinazoshiriki ni:

  1. Zanzibar Heroes (wenyeji)
  2. Kilimanjaro Stars (wenyeji pacha)
  3. Timu ya Taifa ya Burundi
  4. Timu ya Taifa ya Uganda
  5. Timu ya Taifa ya Kenya
  6. Timu ya Taifa ya Burkina Faso

Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo ataondoka na zawadi nono ya shilingi milioni 100.

Kocha na Mkakati wa Kikosi

Ahmed Ally, kocha wa timu ya JKT Tanzania, amepewa jukumu la kuiongoza Kilimanjaro Stars kwenye michuano hii. Akizungumza baada ya uteuzi wake, Kocha Ahmed alisema:

“Ni nafasi nzuri nimeipata, nawashukuru viongozi kwa kuona kitu kutoka kwangu. Baada ya kupewa majukumu haya, nimekaa na wenzangu na kuita kikosi tunachoamini ni imara kitakachofanya vizuri katika mashindano hayo.”

Kocha Ahmed Ally pia alieleza kuwa lengo lake ni kutumia mashindano haya kama sehemu ya maandalizi ya mashindano makubwa yajayo, ikiwemo CHAN na AFCON, huku akizingatia wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Orodha ya Wachezaji wa Kilimanjaro Stars 2025 Watakaoiwakilisha Tanzania

Kikosi kilichoteuliwa na Kocha Ahmed Ally kimejumuisha wachezaji 28 kutoka klabu mbalimbali za Tanzania Bara. Hawa ni wachezaji ambao wanatarajiwa kuonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2025:

  1. Metacha Mnata (Singida BS)
  2. Ramadhani Chalamanda (Kagera Sugar)
  3. Anthony Mpemba (Azam FC, Ngorongoro Heroes)
  4. Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  5. Nickson Mosha (KMC FC, Ngorongoro Heroes)
  6. Vedastus Masinde (TMA Stars, Ngorongoro Heroes)
  7. Lameck Lawi (Coastal Union, Ngorongoro Heroes)
  8. Wilson Nangu (JKT Tanzania)
  9. David Bryson (JKT Tanzania)
  10. Pascal Msindo (Azam FC)
  11. Hijjah Shamte (Kagera Sugar, Ngorongoro Heroes)
  12. Semfuko Charles (Coastal Union)
  13. Said Naushad (Kagera Sugar)
  14. Ahmed Bakari Pipino (KMC FC, Ngorongoro Heroes)
  15. Sospeter Bajana (Azam FC)
  16. Abdulkarim Kiswanya (Azam FC, Ngorongoro Heroes)
  17. Idd Nado (Azam FC)
  18. Bakary Msimu (Coastal Union, Ngorongoro Heroes)
  19. Zidane Sereri (Dodoma Jiji, Ngorongoro Heroes)
  20. Ayoub Lyanga (Singida BS)
  21. William Edgar (Fountain Gate)
  22. Nassoro Saadun (Azam FC)
  23. Offen Chikola (Tabora United)
  24. Joshua Ibrahim (KenGold FC)
  25. Abdul Hamis (Azam FC)
  26. Sabri Kondo (KVZ, Ngorongoro Heroes)
  27. Gamba Idd (JKT Tanzania)
  28. Crispin Ngushi (Mashujaa FC)

Kikosi Cha Kilimanjaro Stars Kitakacho Shiriki Mapinduzi Cup 2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025
  2. Timu Zinazoshiriki Mapinduzi cup 2025
  3. Mapinduzi Cup 2025 Kuchezwa na Timu za Taifa Badala ya Vilabu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo