Kikosi cha Azam VS Singida Black Stars Leo 28/11/2024 | Kikosi cha Azam Leo Dhidi ya Singida Black Stars
Wana rambaramba Azam FC leo watashuka dimbani kuwakalibisha Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 ambao umepangwa kutimua vumbi katika dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na mvuto wa kipekee kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote, huku pande zote mbili zikihitaji ushindi ili kuimarisha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.
Azam FC ipo kwenye kiwango bora msimu huu, ikiwa imeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa alama 24, nyuma ya vinara Simba SC wenye alama 28. Timu hiyo imekuwa na safu imara ya ulinzi na ushambuliaji, ikifunga mabao 14 na kuruhusu mabao matatu tu katika mechi 11 za ligi. Chini ya uongozi wa Kocha Mkuu, Rachid Taoussi, Azam imefanikiwa kushinda michezo saba, sare mbili, na kupoteza mmoja tangu ateuliwe mwezi Septemba 2024.
Kwa upande mwingine, Singida Black Stars wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 24 sawa na Azam lakini wakitofautiana kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa. Hata hivyo, mwenendo wao wa hivi karibuni umekuwa wa kusuasua, wakitoka sare tatu mfululizo, jambo lililochangia kusimamishwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Patrick Aussems, na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Nswanzurimo kama kaimu kocha.
Katika safu ya ushambuliaji, Azam FC wanajivunia nyota kama Nassor Saadun, aliyefunga mabao matatu, na wachezaji wengine muhimu kama Idd Seleman ‘Nado’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, na Gibril Sillah, kila mmoja akiwa amepachika mabao mawili msimu huu.
Kwa upande wa Singida Black Stars, kinara wao wa mabao ni Mkenya Elvis Rupia, mwenye mabao manne, akifuatiwa na Marouf Tchakei, mwenye mabao matatu. Katika lango, Mohamed Mustafa wa Azam ana ‘Clean Sheets’ tano, huku Metacha Mnata wa Singida akiwa nazo sita. Hii inaashiria pambano la kiufundi kati ya safu za ulinzi na mashambulizi za timu zote mbili.
Kikosi cha Azam VS Singida Black Stars Leo 28/11/2024
Kikosi rasmi cha Azam kitakacho anza leo dhidi ya Singida Black Stars kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 12 jioni. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Azam Rachid Taoussi.
Changamoto Zinazokabili Timu
Kocha wa Azam, Rachid Taoussi, amekiri kuwa licha ya kiwango bora cha timu yake, safu ya ushambuliaji bado haijakuwa na ufanisi wa kutosha katika kumalizia nafasi nyingi wanazozitengeneza. “Tumekuwa tukipata pointi tatu, lakini tunahitaji kuboresha zaidi eneo la umaliziaji,” alisema Taoussi.
Kwa upande wake, kaimu kocha wa Singida, Ramadhan Nswanzurimo, amesema timu yake imejipanga kimwili na kiakili kukabiliana na Azam, licha ya kuwa na muda mfupi wa maandalizi. “Lengo ni kuhakikisha tunarejea na ushindi, ingawa tunatambua ubora wa wapinzani wetu,” alisema.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Azam VS Singida Black Stars Leo 28/11/2024 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi Za Leo 28/11/2025
- Simba Yafungua Michuano ya Makundi ya CAF kwa Ushindi wa 1-0
- Matokeo ya Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Kikosi cha Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Sababu 10 za 1xBet Kuwa Kipenzi Cha Watanzania Wengi
- Msuva Asubiri Mkataba Mpya Mnono Al-Talaba SC
- Kocha Kagera amsifu Charles Boniface Mkwasa: ‘Kocha bora nchini’
Leave a Reply