Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024

Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024

Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024 | Kikosi cha Azam Leo Dhidi ya Yanga Sc

Wana Rambaramba Azam FC leo watakua wageni katika uwanja wao wa Nyumbani ambapo watakaribishwa na Yanga SC katika moja kati ya mechi zenye ushindani mkubwa Tanzania. Mechi hii, ambayo inajulikana kama Dar es Salaam Derby, ni miongoni mwa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kote nchini. Azam Complex, Dar es Salaam, ndio utakua uwanja wa vita wa pambano hili la kukata na shoka, huku timu zote mbili zikiingia dimbani na lengo moja—kushinda na kudumisha hadhi ya klabu zao.

Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi bora. Mpaka sasa, Yanga SC imecheza mechi nane na kushinda zote, ikiwa na pointi 24 na mabao 13, na cha kuvutia zaidi, hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa hata mara moja. Kocha Gamondi na kikosi chake wameonyesha nidhamu na ubora mkubwa, wakidhamiria kutetea ubingwa wao kwa nguvu zote msimu huu.

Kwa upande wa Azam FC, timu hii inatarajiwa kutumia fursa ya kuwa wenyeji kujaribu kuvunja rekodi ya Yanga SC. Azam FC imekuwa na safari yenye changamoto, hasa baada ya kupoteza fainali mbili mfululizo dhidi ya Yanga—Kombe la FA huko Zanzibar mnamo Juni 2, 2024, na Ngao ya Jamii mnamo Agosti 11. Azam, ikiongozwa na kocha Rachid Taoussi, inatarajia mchezo huu kama nafasi ya kulipiza kisasi na kuonyesha ubora wao kwa mashabiki.

Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024

Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024

Kikosi rasmi cha Azam Fc kitakacho anza leo dhidi ya Yanga Sc kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 11. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Azam Rachid Taoussi.

Hiki Ndicho Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024

Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs Azam Fc Leo 02/11/2024

Kauli za Makocha Kuelekea Derby

Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamondi, amesema kikosi chake kipo tayari kwa changamoto ya leo, licha ya ratiba ngumu waliyokumbana nayo ikiwemo safari ya Zanzibar walipocheza na Singida Black Stars na kushinda 1-0. Gamondi amesisitiza umuhimu wa nidhamu na kuheshimu wapinzani, akibainisha kuwa Azam ni timu yenye uwezo mkubwa, yenye wachezaji na kocha bora.

“Tumesafiri na kurudi hapa Dar es Salaam, na tumefanya maandalizi ya kurudisha utulivu wa mwili,” alisema Gamondi. “Tunajua itakuwa mechi yenye ushindani. Tuna malengo makubwa ya kudumisha ubora wetu, na tunahitaji ushindi ili tuweze kuyatimiza,” aliongeza.

Kwa upande mwingine, Kocha Rachid Taoussi wa Azam FC alitoa tamko kuhusu kikosi chake akisema kwamba wamejiandaa vizuri kwa kutumia falsafa ya klabu yao, huku akitambua ubora wa Yanga SC.

“Hii ni mechi ngumu lakini Azam ni timu kubwa pia hapa Tanzania,” alisema Taoussi. Amejivunia kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu, wengi wao wakiwa ni wachezaji wa kimataifa ambao wamekuwa wakiliwakilisha taifa kwenye mashindano mbalimbali.

Taoussi na Gamondi, ambao wamefanya kazi pamoja huko nyuma, wanasema kuwa urafiki wao hautaathiri ushindani wa mchezo huu, kwani uwanja utakuwa ndio mahali pa kuonyesha ubora wao kwa dakika 90.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga Vs Azam Fc Leo 02/11/2024
  2. Yanga Vs Azam Fc Leo 02/11/2024 Saa Ngapi?
  3. Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC Tanzania 02/11/2024
  4. Ratiba ya Mechi za Leo 02/11/2024
  5. Fountain Gate Yajiandaa Kuikabili Pamba FC Novemba 5
  6. Sopu Kubaki Chamanzi Hadi 2025/2026
  7. Matokeo ya Mashujaa Vs Simba Leo 01/11/2024
  8. Gamondi Aomba Nyota watatu Kuongeza Nguvu kwenye Kikosi Cha Yanga
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo