KenGold Yajipanga Kutingisha Nyavu za Yanga SC Ligi Kuu

KenGold Yajipanga Kutingisha Nyavu za Yanga SC Ligi Kuu

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 unazidi kushika kasi, na sasa macho yote yanaelekezwa Mbeya ambapo KenGold, licha ya kuanza msimu kwa kusuasua, wametoa tamko la kujiamini wakati wakijiandaa kuwakaribisha mabingwa watetezi Yanga SC ambao wamekua na matokeo mazuri katika michezo kadhaa iliopita. Je, huu ni mkwara mtupu au dalili ya mabadiliko ya upepo kwa wenyeji?

KenGold Yajipanga Kutingisha Nyavu za Yanga SC Ligi Kuu

Yanga SC, wakiwa wameanza msimu kwa kasi ya kimbunga, wamefunga jumla ya mabao 24 hadi sasa katika mechi saba za mashindano mbalimbali yakiwemo mashindano ya klabu bingwa CAF, huku wakiruhusu bao moja pekee. Ushindi wao wa hivi karibuni wa 7-0 dhidi ya CBE SA katika Ligi ya Mabingwa Afrika umeonyesha wazi kwamba wako katika kiwango cha juu.

KenGold, licha ya kupoteza mechi zao zote nne za mwanzo wa ligi kuu ya NBC na kocha wao kujiuzulu, wanaonekana kuwa na matumaini mapya chini ya kocha Jumanne Challe. Challe ametoa kauli ya kujiamini, akisema kwamba lolote linawezekana katika soka na kwamba wamejipanga vyema kuwakabili Yanga.

Mchezo huu utakuwa wa kwanza kati ya KenGold na Yanga SC katika historia ya soka ya Tanzania, na hivyo kuongeza msisimko zaidi. Mashabiki wa soka nchini Tanzania watakuwa na hamu ya kuona kama KenGold wataweza kusimamisha wimbi la mashambulizi ya Yanga au kama mabingwa watetezi wataendeleza ubabe wao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Guardiola Atoa Tamko Kali: Wapinzani ‘Wana Roho Mbaya’
  2. Pot za Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2024/2025
  3. Pot za Makundi ya Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  4. Timu zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  5. Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho CAF 2024/2025
  6. Timu zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  7. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo