KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate

KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6 1 Mbele ya Fountain Gate

KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate

Kichapo cha mabao 6-1 ilichopata KenGold kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga SC kimeacha simanzi kubwa kwa timu hiyo. Hasira na machungu vilivyosababishwa na kichapo hicho, wanatarajia kumalizia kwa Fountain Gate FC watakaoumana nao Jumatatu kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

KenGold, ambayo ilifanya usajili wa kishindo katika dirisha dogo, ilishindwa kabisa kuonyesha ubora wao dhidi ya Yanga SC. Kipigo hicho cha 6-1 kimekuwa kikubwa zaidi msimu huu, huku baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa hawakuweza kuonekana uwanjani, ukiondoa wachache kama vile Zawadi Mauya.

Timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu na inaburuza mkia ikiwa na pointi sita baada ya mechi 17, imesema mechi ijayo dhidi ya Fountain Gate ndio kipimo kizuri kuonyesha kama wamezaliwa upya. Mabosi wa klabu hiyo wamewatuliza mashabiki kwamba timu hiyo haitashuka daraja.

KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate

KenGold itakutana na Fountain Gate, timu ambayo ilitoka kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Simba SC. Katika mchezo baina yao duru lililopita, KenGold walipokea kichapo cha 2-1 mjini Manyara, hivyo Jumatatu itakuwa na kazi ya kulipa kisasi ikiwa nyumbani jijini Mbeya.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Omary Kapilima, alisema katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga SC wamebaini kuwa mabeki walipoteza umakini, lakini wapo baadhi ya wachezaji ambao hawakucheza, hivyo mchezo ujao lazima kieleweke.

Alisema katika michezo 13 iliyobaki, watatumia vyema mechi nane watakazocheza nyumbani kutafuta pointi 24 ambazo zitaweza kuwaondoa mkiani na kubaki salama Ligi Kuu.

“Tunaenda kuanza na Fountain Gate, tuna mechi nane nyumbani ambazo kwa hesabu zetu zitaweza kutuvusha kubaki salama Ligi Kuu msimu ujao, suala la kushuka daraja halipo kwa Ken Gold,” alisema Kapilima.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Tanzania (Taifa Stars) Afcon 2025
  2. CAF Yatangaza Ratiba Ya Fainali za Afcon 2025
  3. Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora
  4. Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
  5. Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
  6. CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
  7. Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
  8. Kilichomuondoa Ramovic Yanga Hatimaye Chafichuka
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo