Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC

Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC

Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC

Klabu ya KMC FC imemtangaza rasmi Kali Ongala kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Abdihamid Moalin aliyekuwa akiiongoza timu hapo awali. Uamuzi huu ulitangazwa siku ya Alhamisi ya tarehe 14 Novemba 2024, katika hafla iliyohudhuriwa waandishi wa habari mbalimbali na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Songoro Mnyonge.

Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC

Safari ya Ongala Kufikia Nafasi Hii

Kali Ongala ana historia ndefu katika ulimwengu wa soka, akiwa amepata uzoefu kama mchezaji na kocha. Akiwa mchezaji, Ongala amewahi kuzichezea klabu maarufu kama Azam FC, Yanga SC, na GIF Sundsvall ya Sweden, miongoni mwa nyingine. Baada ya kustaafu uchezaji, alianza safari yake kama kocha ambapo aliwahi kuifundisha Azam FC na hivi karibuni alikuwa akifundisha kikosi cha vijana cha Timu ya Taifa ya Tanzania U-20.

Katika hafla ya utambulisho wake, Mheshimiwa Songoro Mnyonge alisema:

“Baada ya kikao cha Bodi kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa kocha Abdihamid Moalin, kikao kilichambua CV za makocha mbalimbali na kumchagua Kali Ongala kama kocha bora wa kuiongoza KMC FC.”

Matarajio ya Kali Ongala

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kali Ongala alielezea furaha yake kwa nafasi hiyo mpya:

“Licha ya kupokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali, nilivutiwa sana na mpango wa KMC FC. Matarajio yangu ni kuhakikisha timu inamaliza msimu huu ikiwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.”

Ongala ameweka wazi dhamira yake ya kujenga kikosi imara ambacho kitakuwa na uwezo wa kushindana kwa ufanisi dhidi ya timu nyingine kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ethiopia Vs Tanzania 16/11/2024 Saa Ngapi?
  2. Gamondi Akalia Kuti Kavu Yanga
  3. Kikosi cha Tanzania Vs Ethiopia 16/11/2024
  4. Simba Queens yaendeleza ubabe Soka la Wanawake
  5. Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
  6. Tabora United Waahidiwa Tsh Milioni 50 Kuifunga Simba
  7. Taifa Stars Kuiendea mechi Dhidi ya Ethiopia Kimkakati
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo