Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole

Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole

Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole

Juhudi za Kagera Sugar za kuinasa saini ya aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2021/2022, George Mpole, hatimaye zagonga mwamba. Klabu hiyo imethibitisha kufunga rasmi juhudi za kumsajili mshambuliaji huyo kwa kile ilichosema ni kuepuka kuathiri utulivu wa hesabu zao katika harakati za kubaki Ligi Kuu. Kagera Sugar ilimsajili George Mpole kwa mkopo kutoka Pamba Jiji ya Mwanza kupitia dirisha dogo la usajili msimu huu. Hata hivyo, mshambuliaji huyo ameshindwa kujiunga na timu hiyo kwa wakati, hali iliyosababisha uongozi wa Kagera kuchukua hatua ya kusitisha mpango huo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, sababu kubwa ya kushindikana kwa dili hilo ni kutokufikia makubaliano mazuri kati ya mchezaji na uongozi wa Kagera Sugar. Mpole alidai kuwa angejiunga na klabu hiyo mara tu baada ya kuingiziwa fedha walizokubaliana, lakini hali ilibadilika kutokana na vikwazo vilivyojitokeza katika mazungumzo.

Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole

Kagera Sugar Yachoka na Usumbufu

Viongozi wa Kagera Sugar wameeleza kuwa mazungumzo yao na Mpole yalikuwa na changamoto nyingi, jambo lililopelekea wao kuamua kusitisha mchakato wa kumsajili.

“Kweli tulikuwa tunamuhitaji lakini tumeona mambo yanakuwa mengi. Mara leo anataka hili, kesho mambo yanabadilika. Umekuwa ni usumbufu mkubwa, tumeamua kumuachia afanye maamuzi yake,” alisema mmoja wa viongozi wa Kagera Sugar.

Aidha, klabu hiyo imeeleza kuwa kwa sasa wanajikita zaidi katika kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu, huku wakiona kuwa kuendelea kuhangaika na usajili wa mchezaji mmoja sio maamuzi sahihi katika hali waliyopo.

George Mpole Bado Hajarudi Pamba Jiji

Licha ya kwamba usajili wake Kagera Sugar umekwamishwa, bado haijafahamika hatima ya George Mpole, kwani hajarejea rasmi Pamba Jiji ya Mwanza. Hali hii inaacha maswali mengi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo, huku wadau wa soka wakisubiri kuona ni wapi atakwenda kuendelea na taaluma yake.

Kwa sasa, Kagera Sugar inaendelea na maandalizi ya mechi zake za Ligi Kuu huku ikiweka mkazo kwenye wachezaji waliopo kikosini ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika harakati zao za kusalia kwenye ligi hiyo msimu huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la FA 2024/2025 England
  2. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
  3. Haaland na Marmoush Waipeleka Man City Nusu Fainali FA Cup
  4. Nyota Wa Real madrid Hatiani Kuikosa Robo fainali UEFA Dhidi ya Arsenal
  5. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025
  6. Kikosi Cha Simba kilichosafiri kwenda misri kucheza dhidi ya Al Masry
  7. Yanga SC Yatinga Robo Fainali Kombe la FA Baada ya Kuichapa Songea United
  8. Kikosi cha Yanga vs Songea United Leo 29/03/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo