Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania

Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania | Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima & Mtoto Chini Ya miaka 10

Cheti cha kuzaliwa ni hati muhimu sana sio tu nchini Tanzania bali Duniani kote. Cheti hiki ndicho kinatumika kama ushahidi rasmi wa kuzaliwa kwa mtu, kikionyesha taariza zote za mtu husika kuanzaia tarehe, mahali, na wazazi wake. Hati hii hutumika katika nyanja mbalimbali za maisha, kuanzia kutambulisha mtu, kusafiri, kupata ajira, mashuleni hadi kufungua akaunti za benki.

Licha ya umuhimu uliopo wa kuwa na cheti za kuzaliwa na wengi hujikuta wakifanya michakato ya kuwatengenezea watoto wao mara tu baada ya kuzaliwa, wapo watu ambao hawakuweza kupata kutengenezewa cheti hiki pindi wakiwa watoto (baada ya kuzaliwa). Hii inaweza kuwa kutokana na sababu mbalimbali, kama vile kutokuwepo kwa ufahamu wa umuhimu wa usajili, ugumu wa kufikia katika ofisi za usajili wa vyeti hivi, au kupoteza cheti cha awali cha kuzaliwa.

Kukosa cheti cha kuzaliwa kunaweza kuleta changamoto nyingi kwa mtu mzima. Inaweza kumzuia kushiriki kikamilifu katika huduma mbalimbali za kijamii, kupata huduma muhimu kama vile elimu au bima ya Afya, au hata kuthibitisha uraia wake. Kwa hiyo, ni muhimu kwa kila mtu mzima asiyekuwa na cheti cha kuzaliwa kuchukua hatua za kupata hati hii muhimu.

Mwongozo huu umetolewa ili kuwasaidia watu wazima nchini Tanzania kupata cheti cha kuzaliwa. Utawaelekeza katika mchakato mzima, kuanzia aina za vyeti vya kuzaliwa, mahitaji, utaratibu wa maombi, hadi changamoto zinazoweza kutokea na jinsi ya kuzitatua.

Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima & Mtoto

Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima & Mtoto

Utaratibu wa kupata cheti cha kuzaliwa hutofautiana kulingana na muda uliopita tangu mtoto kuzaliwa. Hapa tumekuleta muongozo wenye maelezo ya kina kuhusu jinsi ya kupata cheti za kuzaliwa kulingana na siku zilizopita tangu kuzaliwa.

1. Kupata Cheti Cha Kuzaliwa kwa Mtoto Aliezaliwa Ndani ya Siku 90

Utaratibu wa kupata cheti cha kuzaliwa kwa ajili ya mtoto ambae amezaliwa ndani ya siku 90 ni wa haraka na rahisi kwa wale walio na taarifa kamili za kuzaliwa. Ili kuanza mchakato wa kuomba cheti cha kuzaliwa fuata utaratibu hapa chini

  1. Kizazi Hospitalini/Kituo cha Afya/Zahanati: Mzazi au mlezi atahitajika kuhakikisha amepewa “Tangazo la Kizazi” kutoka kwa mtoa huduma wa afya kabla ya kuondoka katika kituo husika.
  2. Kizazi Nyumbani: Iwapo mtoto alizaliwa nyumbani, mzazi au mlezi anapaswa kutoa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa Vizazi na Vifo wa wilaya ndani ya siku 90 tangu kuzaliwa. Taarifa hii itasaidia katika kupata “Tangazo la Kizazi.”
  3. Wasilisha “Tangazo la Kizazi”: Baada ya kupata “Tangazo la Kizazi,” mzazi au mlezi anatakiwa kuwasilisha hati hii kwa Msajili wa Vizazi na Vifo wa wilaya ambapo mtoto alizaliwa.
  4. Lipa Ada: Mzazi au mlezi atatakiwa kulipa ada ya usajili ambayo kwa sasa ni shilingi 8,000/=. Baada ya malipo, cheti cha kuzaliwa kitatolewa.

2. Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtoto mwenye Siku 90 Lakini Chini ya Miaka 10

Utaratibu huu unahusisha hatua zaidi ikilinganishwa na usajili wa ndani ya siku 90.

Fomu ya Maombi: Mzazi au mlezi anatakiwa kujaza na kuwasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3. Fomu hii inapatikana katika ofisi za Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA) au ofisi za serikali za mitaa.

Picha: Mzazi au mlezi anatakiwa kuambatanisha picha ya mtoto (passport size) kwenye fomu ya maombi.

Nyaraka za Ushahidi: Ili kuthibitisha taarifa za kuzaliwa, mzazi au mlezi anatakiwa kuambatanisha nyaraka kama vile:

  • Pasipoti
  • Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au sekondari
  • Kadi ya kliniki ya mtoto
  • Cheti cha ubatizo (ikiwa inafaa)
  • Barua kutoka ofisi za serikali (mfano, ofisi ya mtendaji wa kata/kijiji)

Ada ya Usajili: Baada ya kuwasilisha fomu na nyaraka, mzazi au mlezi atalipa ada ya usajili ambayo kwa sasa ni shilingi 8,000/=.

3. Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima Zaidi ya Miaka 10

Utaratibu huu unahitaji umakini zaidi na nyaraka za ziada kutokana na muda mrefu uliopita.

Fomu ya Maombi: Mzazi au mlezi hujaza na kuwasilisha Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3. “Bofya Hapa Kupakua Fomu

Picha: Picha ya mtoto (passport size) inahitajika.

Nyaraka za Ushahidi: Mzazi au mlezi anatakiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kama vile:

  • Kadi ya kliniki ya mtoto
  • Cheti cha ubatizo (ikiwa kipo)
  • Barua kutoka mamlaka za serikali (mfano, ofisi ya mtendaji wa kata/kijiji)
  • Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au sekondari

Nyaraka za Utambulisho (kwa waliozaliwa zamani): Kwa wale waliozaliwa miaka mingi iliyopita, wanatakiwa kuambatanisha nyaraka za ziada kama vile:

  • Kadi ya Utaifa pamoja na Kadi ya Kura au Bima ya Afya.
  • Leseni ya Gari (lazima iambatane na Kadi ya Utaifa au Kadi ya Kura).

Ada ya Usajili: Ada ya usajili kwa utaratibu huu ni shilingi 20,000/=.

Mapendekezo ya mhariri:

  1. Jinsi Ya kukata Tiketi Ya Treni Online (eticketing.trc.co.tz) 2024
  2. Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024
  3. Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Online 2024
  4. Jinsi Ya Kukopa Salio Nipige Tafu Vodacom (Menu Ya Kukopa Salio Vodacom) 2024
  5. Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
  6. Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Biashara Ya Duka La Rejareja
  7. Jinsi Ya Kuangalia Taarifa Zangu Za NIDA 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo