Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025

Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025: Katika jitihada za kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao wa 2024/2025, klabu ya Simba SC imeingia katika hatua za mwisho za kumsajili kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua kutoka Ivory Coast. Ahoua anatarajiwa kurithi mikoba ya Clatous Chama, ambaye amehamia Yanga SC baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

Usajili wa aliekua mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Simba, Chama Cloutus umezua hisia tofauti kwa mashabiki wa Simba sababu wengi wanaamini klabu bado ilikua inahitaji huduma ya staa uyo ambae amekua katika ubora mkubwa tangu kujiunga na Simba.

Msemaji wa klabu ya Simba, amewataka mashabiki wa Simba kuwa na imani na benchi lao  la ufungu sababu wapo kwenye mchakato wa kuleta nyota wengine ambao wanauwezo mkubwa zaidi na wenye umri mdogo na nguvu.

Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025

Jean Charles Ahoua, mwenye umri wa miaka 22, amekuwa mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya Ivory Coast akiwa na Klabu ya Stella Club d’Adjame. Katika msimu wa 2023/2024, Ahoua alifunga mabao 12 na kutoa pasi 9 za mabao, hivyo kushiriki katika mabao 21 kwa jumla. Uwezo wake wa kucheza kama kiungo mshambuliaji wa namba 10 umevutia wengi, ikiwemo uongozi wa Simba SC.

Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025

Safari ya Ahoua Kuja Simba

Habari kutoka ndani ya klabu ya Simba na vyanzo vya kuaminika kutoka Afrika Magharibi zinaeleza kuwa Ahoua atasafiri kutoka Ivory Coast kuja Tanzania kukamilisha usajili wake. Tayari kila kitu kimekamilika na kilichobaki ni yeye kutua na kusaini mkataba wa miaka mitatu kabla ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Simba SC.

Matarajio ya Mashabiki wa Simba kwa Ahoua

Kusajiliwa kwa Ahoua kunaleta matumaini makubwa kwa klabu ya Simba, hasa baada ya uongozi kuamua kumuacha Clatous Chama kutokana na changamoto za kinidhamu na umri wake. Mtoa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo alibainisha kuwa Ahoua ni mchezaji mwenye nidhamu na uwezo mkubwa, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Chama na kuisaidia timu kurudisha makombe.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa klabu hiyo inaendelea na usajili wa wachezaji wapya na tayari kuna wachezaji saba wa kigeni waliopo nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili. Ahmed amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa na subira na kuwaahidi kuwa timu inajengwa upya ili kurudisha furaha na heshima ya klabu hiyo.

Mpango Mkakati wa Simba 2024/2025

Kwa mara ya kwanza baada ya misimu mingi, Simba SC inatarajia kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wapya katika kikosi chake. Uongozi wa klabu unafanya mabadiliko makubwa ili kutengeneza timu mpya itakayoweka rekodi nzuri na kuleta makombe. Hili linafanyika makusudi ili kuhakikisha Simba SC inarudi katika nafasi yake ya juu na kuleta furaha kwa mashabiki wake.

Hitimisho

Usajili wa Jean Charles Ahoua unatarajiwa kuwa hatua muhimu kwa Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025. Mashabiki wa Simba wana matumaini makubwa kwa nyota huyu mpya na wanaamini kuwa atarithi mikoba ya Chama na kuisaidia timu yao kupambana na kuleta ushindi. Ahoua anaingia Simba SC akiwa na lengo moja tu, kurudisha heshima na furaha kwa klabu hiyo kubwa nchini Tanzania.

Mapendekezzzo Ya Mhariri:

  1. Cv Ya Steven Mukwala Mchezaji Mpya Wa Simba 2024/2025
  2. Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
  3. Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
  4. Tetesi za Usajili simba 2024/2025
  5. Wachezaji Wapya Simba 2024/2025
  6. Simba Day 2024: Tarehe Rasmi Yatangazwa na Simba SC
  7. Mishahara Ya Wachezaji Wa Simba 2024/2025
  8. Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo