Ifahamu CBE SA Ya Ethiopia Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa

Ifahamu CBE SA Ya Ethiopia Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa

Baada ya kuifanyia uzalilishaji wa hali ya juu klabu ya Vital’o ya Burundi, mabingwa soka nchini Tanzania Yanga sasa watakutana na klabu ya CBE SA ya Ethiopia katika roundi ya pili ya hatua za awali za michuano ya klabu bingwa Afrika CAF. Hapa tumekusanyia na kukuletea taarifa zote kuhusu klabu ya CBE SA ili uweze kufahamu vizuri zaidi wapinzani wa Yanga.

Historia ya Klabu ya CBE SA

CBE SA, inayojulikana pia kwa jina la Ethiopia Nigd Bank, ni klabu ya soka kutoka Ethiopia yenye makao yake jijini Addis Ababa. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1982 ikiwa inajulikana kama Banks SC kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2010 na kuitwa Commercial Bank of Ethiopia Sports Association (CBE SA), jina ambalo wanatumia hadi sasa.

CBE SA ni moja ya klabu zinazoongoza katika soka la Ethiopia. Wana historia ya mafanikio katika ligi kuu ya Ethiopia, wakitwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa 2023/24. Pia, klabu hii imewahi kushinda taji la Addis Ababa City Cup mwaka 2014. Mafanikio haya yameifanya CBE SA kuwa moja ya klabu zenye nguvu nchini Ethiopia.

Ifahamu CBE SA Ya Ethiopia Wapinzani wa Yanga Klabu Bingwa

Uwanja wa Nyumbani

Klabu ya CBE SA inatumia Uwanja wa Addis Ababa kwa michezo yake ya nyumbani. Uwanja huu ni mojawapo ya viwanja maarufu nchini Ethiopia, wenye uwezo wa kupokea idadi kubwa ya mashabiki, na unajulikana kwa kuandaa mechi za kiwango cha juu.

Ushiriki wa Kimataifa

CBE SA inaingia kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yake msimu huu. Hapo awali, klabu hii imeshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mara mbili, lakini hawakufanikiwa kufika hatua ya makundi. Wameshiriki mara mbili tu katika Kombe la Shirikisho barani Afrika, mwaka 2005 na 2010, ambapo waliondolewa katika raundi ya kwanza.

Kikosi cha CBE SA

Kikosi cha CBE SA kimejaa vipaji vya wachezaji wazuri kama Basiru Umar, Fetudin Jemal, Kitika Jema, na Fuad Fereja. Hawa ndio wachezaji wa kutazamwa zaidi kwenye mechi zao dhidi ya Yanga, kwani wana uwezo wa kubadili mchezo wakati wowote.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  2. Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024
  3. Yanga Kucheza na CBE SA Ya Ethiopia Klabu Bingwa Septemba 2024
  4. Coastal Union Yatolewa Kombe la Shirikisho CAF
  5. Usajili wa Mukwala na Ahou Waanza Kulipa Msimbazi
  6. Matokeo Simba Vs Fountain Gate Leo 25/08/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo