Huu Apa Utaratibu wa Droo ya Makundi CAF, Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho 2024/25
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetangaza rasmi utaratibu wa droo ya hatua ya makundi kwa michuano ya TotalEnergies CAF Champions League almaharufu kama klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2024/25. Tukio hili la droo ni muhimu sana katika kuelekea hatua ya makundi ya michuani hii kwani linaamua safari ya vilabu vinavyoshiriki michuano hii mikubwa barani Afrika. Makundi haya yanajumuisha vilabu bora kutoka mataifa mbalimbali, vikikabiliana kwa lengo la kuibuka mabingwa wa Afrika.
Tarehe na Mahali Droo ya Makundi CAF Inafanyika
Droo ya hatua ya makundi itafanyika Jumatatu, tarehe 7 Oktoba 2024, jijini Cairo, Misri. Hii itakuwa ni droo ya kuvutia sana kwani mashabiki na wapenzi wa soka kutoka pembe zote za Afrika watakuwa wakisubiri kwa hamu kuona timu zao zitakavyopangwa.
Ratiba ya droo ni kama ifuatavyo:
- Saa 14:00 kwa saa za Afrika Mashariki: Droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho (TotalEnergies CAF Confederation Cup).
- Saa 15:00 kwa saa za Afrika Mashariki: Droo ya makundi ya Klabu Bingwa (TotalEnergies CAF Champions League).
Vilabu Vilivyofuzu Hatua ya Makundi – CAF Champions League
Vilabu 16 tayari vimefuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa kwa msimu huu. Vilabu hivi vinajumuisha mabingwa na washindi kutoka ligi mbalimbali za bara la Afrika. Orodha ya vilabu vilivyofuzu ni kama ifuatavyo:
- Al Ahly SC (Misri)
- Al Hilal SC (Sudani)
- AS FAR (Morocco)
- AS Maniema Union (DR Congo)
- CR Belouizdad (Algeria)
- Djoliba AC De Bamako (Mali)
- GD Sagrada Esperança (Angola)
- Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
- MC Alger (Algeria)
- Pyramids FC (Misri)
- Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- Raja Casablanca (Morocco)
- Stade d’Abidjan (Côte d’Ivoire)
- TP Mazembe (DR Congo)
- Young Africans SC (Tanzania)
Tazama hapa Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho CAF 2024/2025
Utaratibu wa Droo ya Makundi CAF 2024/2025
Droo ya hatua ya makundi itafuata utaratibu ambapo timu zitapangwa kwenye makundi manne (A, B, C, na D) kulingana na nafasi zao kwenye viwango vya CAF. Timu zitatenganishwa kwenye ‘pots’ nne, kila ‘pot’ ikiwa na vilabu vinne.
Pot 4 (Timu za Viwango vya Chini)
Timu zilizomo kwenye Pot 4 ni zile zinazoshikilia viwango vya chini zaidi kulingana na orodha ya CAF. Timu hizi ni kama ifuatavyo:
- MC Alger (Algeria)
- AS Maniema Union (DR Congo)
- Djoliba de Bamako (Mali)
- Stade d’Abidjan (Côte d’Ivoire)
Kila timu katika Pot 4 itapangwa moja kwa moja kwenye kundi. Utaratibu wa droo utaanza na timu kutoka Pot 4 kupewa nafasi za mwisho kwenye kila kundi. Mfano:
- Timu ya kwanza kutoka Pot 4 itapangwa kwenye Kundi A, nafasi ya A4.
- Timu ya pili itapangwa kwenye Kundi B, nafasi ya B4, na kuendelea hadi Kundi D.
Pot 3 (Timu za Kati)
Pot 3 inajumuisha vilabu vinavyojulikana lakini vina viwango vya kati kwenye michuano ya CAF. Vilabu hivi ni:
- Al Hilal (Sudani)
- Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- GD Sagrada Esperança (Angola)
- AS FAR (Morocco)
Utaratibu wa droo utahusisha timu hizi kupewa nafasi ya tatu kwenye makundi husika.
Pot 2 (Timu za Juu)
Vilabu vilivyopo kwenye Pot 2 ni vile vinavyojulikana kwa historia nzuri kwenye michuano ya Afrika, lakini havijafikia viwango vya juu kabisa. Vilabu hivi ni:
- CR Belouizdad (Algeria)
- Raja Casablanca (Morocco)
- Young Africans (Tanzania)
- Pyramids FC (Misri)
Timu za Pot 2 zitapewa nafasi ya pili kwenye makundi A, B, C, na D, kulingana na mpangilio wa droo.
Pot 1 (Timu za Juu Kabisa)
Pot 1 inajumuisha vilabu bora zaidi kwenye viwango vya CAF, vilivyopata mafanikio makubwa barani Afrika. Timu hizi ni:
- Al Ahly SC (Misri)
- Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
- TP Mazembe (DR Congo)
Timu hizi zitapewa nafasi za kwanza kwenye kila kundi, na hivyo kuongoza vikundi vyao katika michuano hii ya Klabu Bingwa.
Droo ya Kombe la Shirikisho
Mbali na Klabu Bingwa, droo ya Kombe la Shirikisho nayo inatarajiwa kufuata utaratibu kama huo. Vilabu vilivyofuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho vitapangwa kwenye makundi manne, yakifuata utaratibu wa droo sawa na ule wa Klabu Bingwa. Hii ni fursa kwa vilabu vidogo kuonesha uwezo wao na kuwania nafasi ya kushinda taji la Kombe la Shirikisho.
Fuatilia Hapa Droo Mubashara
TAZMA HAPA
Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025 (Caf Confederation Cup Groups)
Makundi ya Klabu Bingwa Africa 2024/2025 (Caf Champions League Groups)
Mapendekezo ya Mhariri:
- Pot za Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2024/2025
- Pot za Makundi ya Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Makundi CAF 2024/2025
- Simba Yafuzu Makundi Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
- Ishu ya Joshua Mutale na Jezi ya Kombe la Shirikisho CAF
- CAF Yaagiza Uchunguzi Dhidi ya Vurugu Walizofanyiwa Simba Libya
Leave a Reply