Hizi Apa Code za Haloteli: Namba Muhimu Za Haloteli 2024

Hizi Apa Code za Haloteli: Namba Muhimu Za Haloteli 2024

Halotel ni miongoni mwa mitandao ya simu inayoongoza nchini, ikihudumia kwa gharama nafuu. Imejipatia sifa kwa huduma bora na bei nafuu ikilinganishwa na wengine, hivyo kuwavutia wengi kutumia mtandao huu. Ikiwa wewe ni mteja wa Halotel au unapanga kuanza kutumia mtandao huu, ni muhimu kufahamu Code za Halotel, ambazo ni namba maalum zinazowawezesha wateja wa haloteli kujiunga na huduma mbalimbali. Hapa tumekuletea namba zote za kujiunga na huduma mbalimbali za Haloteli.

Hizi Apa Code za Haloteli: Namba Muhimu Za Haloteli 2024

Code Za Haloteli Huduma
*148*66# Kusajili vifurushi
*148*55# Kusajili vifurushi kwa laini za Chuo, Tomato, Edu na Study
*150*88# HaloPesa
*102# Kuangalia salio Kuu na Ia Ziada
*102*01# Kuangalia salio Ia Promosheni
*106# Kuangalia taarifa za usajili
*15042*1# Kusajili huduma za roaming
namba za *kiasi # *101* mpokeaji Kutuma salio

Hizi Apa Code za Haloteli: Namba Muhimu Za Haloteli 2024

Kuhusu Halotel Tanzania

Halotel ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayojulikana kwa huduma za sauti, ujumbe, data, na mawasiliano nchini Tanzania. Ni mali ya Viettel Global JSC, kampuni ya uwekezaji inayomilikiwa na serikali ya Vietnam, ambayo imekuwa ikifanya uwekezaji katika sekta ya mawasiliano katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Viettel imewekeza zaidi ya dola bilioni moja katika soko la mawasiliano la Tanzania. Halotel ilikuwa kampuni ya kwanza nchini Tanzania kuruhusiwa kuweka miundombinu yake ya fiber optic, na sasa inatoa huduma za mawasiliano katika mikoa yote 26 ya Tanzania, ikiwa na mtandao wa zaidi ya kilomita 18,000 za fiber optic

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
  2. Jinsi ya Kukopa Salio Tigo (Menu Ya Kukopa Salio Tigo) 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo