Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2-1

Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2 1

Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2-1

Hispania imetawazwa mabingwa wa michuano ya UEFA Euro 2024 baada ya kuichapa Uingereza mabao 2-1 katika fainali iliyopigwa Jumapili mjini Berlin. Ushindi huu unaiweka Hispania kileleni kwa kutwaa taji hili kwa mara ya nne, rekodi inayowafanya kuwa nchi yenye mafanikio zaidi katika historia ya michuano hii.

Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2-1

Hispania Yaibuka Mabingwa wa EURO 2024 Baada ya Kuichapa Uingereza 2-1

Katika kipindi cha kwanza, timu zote zilionekana kucheza kwa tahadhari huku Hispania ikimiliki mpira zaidi lakini ikishindwa kupata bao. Hata hivyo, mambo yalibadilika mara baada ya kipindi cha pili kuanza.

Dakika mbili tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Lamine Yamal, kijana mwenye umri wa miaka 17 aliyeibuka kuwa nyota wa michuano hii, alipokea mpira kutoka upande wa kulia. Yamal alishambulia katikati ya uwanja na kutoa pasi murua kwa Nico Williams aliyekuwa akipiga mbio upande wa kushoto wa boksi la adhabu. Williams alimalizia kwa ustadi mkubwa na kuifungia Hispania bao la kwanza.

Uingereza ilisawazisha dakika ya 73 kupitia mpira mzuri wa Bukayo Saka ambaye alipiga krosi na kumkuta Jude Bellingham katika eneo la hatari. Bellingham alirudisha mpira nje ya boksi kwa Cole Palmer aliyepiga shuti kali la mguu wa kushoto na kutinga wavuni.

Hispania ilipata bao la ushindi dakika ya 86 kupitia kwa Mikel Oyarzabal aliyefunga baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Marc Cucurella. Uingereza ilijaribu kurudi mchezoni kwa mashambulizi ya dakika za mwisho, lakini juhudi za Declan Rice na Marc Guehi zilikwama baada ya mashuti yao kuzuiliwa.

Hispania imefanikiwa kutwaa taji la Euro kwa mara ya nne, baada ya awali kushinda mwaka 1964, 2008, na 2012. Mafanikio haya yanazidi kuimarisha nafasi yao kama moja ya timu bora kabisa barani Ulaya.

Katika michuano hii, Hispania haikupoteza mechi yoyote, ikishinda michezo saba na kufunga mabao 15 huku ikiruhusu mabao manne pekee. Michuano hii pia ilikuwa ni jukwaa la kuibuka kwa nyota kijana, Lamine Yamal, ambaye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika historia ya Euro baada ya kufunga bao safi dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali.

Kauli za Wachezaji na Makocha

Nico Williams alisema, “Nina furaha kubwa. Tumestahili ushindi huu. Mashabiki wetu, familia zetu, na kila mtu aliyekuwa akituunga mkono kila siku. Na hapa tupo, mabingwa wa Ulaya. Nimefurahi sana na natumai tutazidi kusonga mbele na kwenda kushinda Kombe la Dunia.”

Nahodha wa Uingereza, Harry Kane, alimpongeza Yamal kwa kusema, “Yeye ni mchezaji mzuri sana. Katika umri wa miaka 17, kufanya hivi kwenye michuano kama hii ni jambo kubwa. Unaweza kuona anacheza bila hofu, kwa uhuru, akifurahia mchezo. Atakuwa miongoni mwa wachezaji wenye changamoto kubwa katika mechi. Nataka kumpongeza kwa alichokifanya hadi sasa.”

Mapendekezo ya mhariri:

  1. Wafungaji Bora EURO 2024: Hawa Ndio Vinara Wa Magoli
  2. England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024
  3. Timu Zilizofuzu Robo Fainali EURO 2024 & Ratiba
  4. Msimamo Makundi ya EURO 2024
  5. Matokeo Ya Mechi Za Euro 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo