Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035

Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035

Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake

Serikali ya Hispania imepania kuandika historia kwa kutaka kuandaa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2035 kwa ushirikiano baina ya Ureno na Morocco. Hayo yalifichuliwa mwaka 2021 baada ya ziara ya ghafla ya Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez, kwenda nchini Morocco ili kuzungumza na Mfalme wa taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika. Sasa, Hispania imechukua hatua nyingine kubwa kwa kushirikiana tena na Morocco na Ureno katika jitihada za kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake mwaka 2035.

Hispania, Morocco na Ureno Wataka Kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake 2035

Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) lilitangaza rasmi azma hiyo siku ya Ijumaa, likieleza kuwa hatua hii inalenga kuendeleza na kuinua hadhi ya michezo ya wanawake duniani. Rais wa RFEF, Rafael Louzan, alithibitisha kuwa tayari kuna juhudi zinazofanyika kuhakikisha kuwa Hispania, Morocco, na Ureno zinakuwa wenyeji wa mashindano hayo makubwa ya soka la wanawake.

“There is no better way to raise the profile of women’s sport than by participating in the most important sporting event in the world, a Fifa World Cup. We are currently working on it,” alisema Louzan alipokuwa akihudhuria kongamano katika Chuo Kikuu cha Madrid. Kauli yake inaonyesha dhamira ya RFEF kuunga mkono maendeleo ya soka la wanawake kupitia uandalizi wa michuano hiyo mikubwa.

Hata hivyo, juhudi hizi pia zinakuja wakati ambapo RFEF inajaribu kurejesha heshima yake baada ya misukosuko kadhaa ya kiutawala katika miaka ya hivi karibuni. Shirikisho hilo limekuwa likikumbwa na matatizo, hasa baada ya aliyekuwa rais wake, Luis Rubiales, kujiuzulu kwa aibu mnamo Septemba 2023. Rubiales alihusika katika kashfa ya kumbusu kwa nguvu mchezaji Jenni Hermoso baada ya Hispania kushinda Kombe la Dunia la Wanawake mwaka huo huko Sydney, Australia.

Baada ya Rubiales, Pedro Rocha alichukua nafasi kwa muda, lakini naye alisimamishwa kwa madai ya kuzidisha mamlaka yake kinyume cha taratibu. Hatimaye, mnamo Desemba 2024, Rafael Louzan aliteuliwa kuchukua nafasi ya uongozi wa RFEF, akiahidi kurejesha heshima na ufanisi ndani ya shirikisho hilo.

Ushirikiano wa Hispania na Morocco pamoja na Ureno si jambo jipya, kwani mataifa haya tayari yanashirikiana kuandaa Kombe la Dunia la Wanaume la mwaka 2030. Katika mashindano hayo, hatua ya makundi ya awali itachezwa nchini Uruguay, Argentina, na Paraguay ili kuadhimisha miaka 100 tangu kufanyika kwa Kombe la Dunia la kwanza mwaka 1930.

Hispania, Morocco, na Ureno sasa wanatarajia kuandika historia nyingine kwa kuwa wenyeji wa mashindano ya wanawake mwaka 2035. Ikiwa ombi lao litakubaliwa, basi itakuwa ni fursa adhimu kwa nchi hizi kuonyesha maendeleo yao katika uandaaji wa mashindano makubwa ya soka, huku ikiendelea kuinua hadhi ya soka la wanawake duniani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Aishi Manula Bado Mambo Magumu Msimbazi
  2. Kane Atazamia Kufikia Rekodi ya Shilton na Kuweka Historia Mpya Uingereza
  3. Yaliyojiri Mkutano wa Waziri Kabudi na TFF, TPLB, Yanga na Simba
  4. CAF Yaondoa Marufuku Uwanja wa Benjamin Mkapa
  5. Sowah Aweka Bayana Nia Yake Yakubeba Kiatu Cha Dhahabu
  6. Majeraha ya Goti Yamkosesha Alphonso Davies Mechi za Mwisho za Msimu
  7. Yanga Yavamia Dili la Fei Simba
  8. Silaha 6 Muhimu za Simba SC Zatangulizwa Misri
  9. Vita ya Top 4 Ligi Kuu Tanzania Bara Yapamba Moto
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo