Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 15/12/2024

kikosi cha yanga vs mashujaa leo

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 15/12/2024

Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Mashujaa leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kimebainishwa rasmi na Kocha Mkuu, Sead Ramovic. Mechi hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Baada ya kushiriki mashindano ya kimataifa, Yanga wanarejea kwenye ligi wakiwa na dhamira ya kuendeleza mbio zao za kutetea ubingwa dhidi ya Mashujaa FC kutoka Kigoma.

Kocha Ramovic amesisitiza kuwa watachukua tahadhari kubwa dhidi ya Mashujaa, ambao ni timu yenye rekodi ya kujihami vizuri. Akizungumza kabla ya mechi, Ramovic alisema: “Najua tunatakiwa kuonyesha uwezo wetu, kila timu tunaiheshimu na kila mechi tunakwenda na mipango tofauti. Lengo letu ni kushinda na kujiweka katika nafasi salama kwenye msimamo wa ligi.”

Kikosi cha Kwanza (Starting XI)

  • Khomeiny
  • Yao
  • Kibuana
  • Job (C)
  • Bacca
  • Aucho
  • Mzize
  • Abuya
  • Dube
  • Aziz Ki
  • Pacome

Wachezaji wa Akiba (Substitutes): Msheri, Kibabage, Mwamyeto, Boka, Nkane, SureBoy, Sheikhan, Faridi M, Moses & Mudathir

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Vs Mashujaa Leo 15/12/2024

Mechi hii ni ya tatu kati ya Yanga na Mashujaa katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo katika michezo miwili ya awali, Yanga walifanikiwa kushinda. Yanga wapo na rekodi ya kushinda michezo mitatu kati ya mitano ya mwisho, huku Mashujaa wakitoka sare mfululizo katika mechi zao tatu za mwisho.

Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa Yanga wamepungukiwa na wachezaji muhimu kama Clatous Chama, Djigui Diarra, Maxi Nzengeli, na Kennedy Musonda, kikosi hiki kimepangwa kwa lengo la kuhakikisha wanapata matokeo chanya licha ya changamoto hizo.

Kocha Ramovic ameongeza kuwa:
“Tunajua umuhimu wa mechi hii na tunaingia kwa lengo moja tu, kuhakikisha tunapata pointi tatu. Tumewaandaa wachezaji wetu vyema kwa mchezo huu.”

Kwa upande wa Mashujaa, Kocha Mohamed Abdallah ‘Bares’ ameahidi kutoa ushindani mkubwa, akibainisha kuwa wachezaji wake wako tayari kwa changamoto hiyo licha ya majeruhi kadhaa waliopo kwenye kikosi chake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga vs Mashujaa leo 19/12/2024
  2. Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)
  3. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  4. Kibu Denis Aipa Simba Ushindi Dhidi ya CS Sfaxien Dakika za Jioni
  5. Matokeo ya Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024
  6. Kikosi cha Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024
  7. Jackson Shiga Anukia Fountain Gate
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo