Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe amepokea kibali cha ajira mpya kutoka kwa katibu mkuu OR – Utumishi chenye Kumbu. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi kwa kada tatu (03) kama zilivyoanishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Yatangaza Nafasi za Kazi (Mwisho 25/07/2024)

Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II (“Office Management Secretary II”) Nafasi 5.

Sifa Za Mwombaji.

kuajiriwa wa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili. aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

Kazi Na Majukumu Ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja La II.

  1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  2. Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  3. Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
  4. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  5. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika idara/kitengo/sehemu husika.
  6. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  7. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali na
  8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Msaidizi Wa Kumbukumbu II (“Records Management Assistant II”) Nafasi 5

Sifa Za Mwombaji.

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (FORM IV) au cha Sita (FORM VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.

  1. Kazi Na Majukumu Ya Msaidizi Wa Kumbukumbu II.
  2. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye rejista (incoming Correspondence register)
  3. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista (outgoing correspondence register)
  4. Kusambaza majalada kwa watendaji (action officers)
  5. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa watendaji.
  6. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji:
  7. Kurudisha majalada kwenye kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
  8. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
  9. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

Mtendaji Wa Kijiji Daraja La Iii – Nafasi 15.

Sifa Za Mwombaji.

Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au Sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA Level 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo:

  • Utawala, Sheria
  • Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

Kazi Na Majukumu Ya Mtendaji Wa Kijiji.

  1. Kuwa Afisa Masuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  2. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji.
  3. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
  4. Kuwa Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
  5. Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu:
  6. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
  7. Kuwa kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika kijiji:
  8. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
  9. Kuwa mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika kijiji
  10. Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji.
  11. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi na;
  12. Atawajibika kwa mtendaji wa kata.

Masharti Ya Ujumla Kwa Waombaji

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  3. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Carriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  4. “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip) HAVITAKUBALIWA.
  5. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  6. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  7. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
  8. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  9. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
  10. Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  11. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  12. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 25 Julai, 2024

Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

  • Mkurugenzi Mtendaji (W),
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
  • 28 Barabara ya Bomani,
  • S.L.P 28001,
  • 61401 Kisarawe,
  • KISARAWE.

Jinsi Ya Kutuma Maombi

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mbogwe (Mwisho Wa Maombi 26 Julai 2024)
  2. Ajira Mpya Shinyanga: Halmashauri ya Manispaa Yatangaza Nafasi mbalimbali – Mwisho wa Kutuma Maombi ni 25 Julai, 2024
  3. Halmashauri ya Mji Handeni Yatangaza Nafasi Mpya za Kazi (Mwisho Julai 27)
  4. Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi: Mwisho wa Maombi Julai 21, 2024
  5. Mwisho wa Kutuma Maombi Ajira Mpya za Afya Zilizotangazwa July 2024
  6. Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II TAMISEMI 2024: Wauguzi 2282 Wahitaji
  7. Ajira za Afya Tanzania 2024: TAMISEMI Yatangaza Nafasi 9,000+!
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo