Haaland Avunja Rekodi ya Rooney ya Magoli EPL

Haaland Avunja Rekodi ya Rooney ya Magoli EPL

Haaland Avunja Rekodi ya Rooney ya Magoli EPL

Erling Haaland, mshambuliaji matata wa Manchester City, ameendelea kuthibitisha ubora wake katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuvunja rekodi ya magoli aliyoweka Wayne Rooney katika msimu wa 2011/12. Katika mechi dhidi ya Brentford, Haaland alifunga magoli mawili, na kufikisha idadi ya magoli tisa ndani ya mechi nne za mwanzo za msimu huu wa EPL (2024/25). Hii ni rekodi mpya katika historia ya EPL, na inampatia nafasi ya kipekee kwenye orodha ya wafungaji bora wa awali wa ligi.

Haaland Avunja Rekodi ya Rooney ya Magoli EPL

Haaland Anafunga Magoli Yasiyokamatika

Katika mechi nne za kwanza za Manchester City, Haaland ameonesha uwezo wa ajabu wa kufunga magoli, akiwa ameweka rekodi mpya ya magoli tisa. Hii inamfanya awe mara tatu zaidi ya mchezaji yeyote aliyefunga magoli mengi katika kipindi hicho cha msimu.

Zaidi ya hayo, Haaland amefunga magoli mawili zaidi ya timu nyingine zote za EPL, ukiondoa klabu yake ya Man City. Kwa takwimu hizi, tayari Haaland yupo mbele sana katika mbio za kuwania tuzo ya kiatu cha dhahabu.

Kuvunja Rekodi ya Wayne Rooney

Kwa magoli yake tisa katika mechi nne, Haaland amevunja rekodi ya Wayne Rooney ambaye alifunga magoli nane katika mechi nne za mwanzo za msimu wa 2011/12 akiwa na Manchester United. Rooney alimaliza msimu huo akiwa na magoli 27, na kwa sasa Haaland tayari ameshafikisha theluthi moja ya idadi hiyo.

Orodha ya wachezaji waliofunga magoli mengi katika mechi nne za kwanza za msimu:

Mchezaji Klabu Msimu Magoli
Erling Haaland Man City 2024/25 9
Wayne Rooney Man Utd 2011/12 8
Diego Costa Chelsea 2014/15 7
Sergio Aguero Man City 2011/12 6
Son Heung-min Spurs 2020/21 6
Dominic Calvert-Lewin Everton 2020/21 6
Erling Haaland Man City 2022/23 6
Erling Haaland Man City 2023/24 6

Kwa sasa, Haaland ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyeweza kufunga magoli mengi zaidi ndani ya mechi tano za kwanza za msimu katika EPL. Magoli yake tisa aliyofunga msimu huu yanalingana na rekodi aliyojiwekea katika msimu wa 2022/23 alipofunga magoli tisa pia.

Haaland ana nafasi nzuri ya kuvunja rekodi yake mwenyewe endapo atafunga goli katika mechi ijayo dhidi ya Arsenal, ambayo itakuwa mechi ya tano ya Manchester City msimu huu.

Rekodi ya Magoli Katika Mechi Tano za Kwanza za EPL

Orodha ya wachezaji waliofunga magoli mengi katika mechi tano za kwanza za msimu wa EPL:

Mchezaji Klabu Msimu Magoli
Erling Haaland Man City 2024/25 9
Erling Haaland Man City 2022/23 9
Wayne Rooney Man Utd 2011/12 9
Sergio Aguero Man City 2011/12 8
Erling Haaland Man City 2023/24 7
Son Heung-min Spurs 2020/21 7
Dominic Calvert-Lewin Everton 2020/21 7
Diego Costa Chelsea 2014/15 7

Hata hivyo, Haaland alikosa nafasi ya kuweka rekodi nyingine ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya EPL kufunga “hat-trick” katika mechi tatu mfululizo. Alikaribia kufunga hat-trick dhidi ya Brentford lakini alipiga mpira kwenye nguzo na pia alipoteza nafasi nyingine kwa kudhibitiwa na kipa wa Brentford, Mark Flekken.

Safari ya Haaland ya Magoli 2024/25

Katika misimu miwili iliyopita, Haaland alifanikiwa kufunga magoli 36 na 27, na hadi sasa, ndani ya mechi nne tu za msimu huu wa 2024/25, tayari ana magoli tisa. Kiasi cha magoli atakayofunga msimu huu bado ni kitendawili, lakini rekodi zake zinaonesha wazi kuwa Haaland ana uwezo mkubwa wa kuvunja rekodi nyingine nyingi zaidi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Azam Fc Yaambulia Sare ya 0-0 Mbele ya Pamba Jiji
  2. Man U Yaishushia Southampton Kichapo cha Goli 3-0
  3. Tabora United Yashindwa Kutamba Nyumbani
  4. Yanga Yaanza na Ushindi Ethiopia, Dube Aingia Wavuni
  5. Matokeo CBE SA vs Yanga Leo 14 September 2024
  6. Jeuri ya Simba Kombe la Shirikisho CAF ipo Hapa
  7. Ubora wa Dube na Pacome Wamfanya Kocha CBE Kuingiwa na Hofu
  8. Goli Pekee la Ngushi Laipa Mashaujaa Ushindi Dhidi ya Coastal Union
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo