Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars

Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars

Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars

STRAIKA wa zamani wa Yanga SC, Joseph Guede, aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Singida Black Stars kabla ya kuondolewa mapema wiki hii, amefunguka kuhusu sababu zilizosababisha kuachana na timu hiyo. Nyota huyo wa Ivory Coast alijiunga na Singida mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kutoka Yanga SC, aliyoitumikia kwa miezi sita kabla ya mkataba wake kusitishwa kwa makubaliano ya pande mbili.

Jeraha Lililomzuia Kuendelea:  Guede ameeleza kuwa changamoto za majeraha ziliathiri sana uwezo wake wa kujituma uwanjani. Akizungumza na Mwanaspoti, Guede alisema:

“Kukaa nje kwa muda nikijiuguza jeraha nililolipata mwanzo wa msimu huu na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, ndiyo sababu iliyoniondoa kwenye kikosi cha timu hiyo.”

Majeraha hayo yalimsababishia kutokuwa na mchango wa moja kwa moja kwa timu, hali iliyomfanya kuachwa nje ya mipango ya Singida Black Stars licha ya matarajio makubwa kutoka kwa mshambuliaji huyo.

Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars

Historia Fupi ya Guede Tanzania

Guede alijiunga na Singida Black Stars baada ya kucheza kwa mafanikio ndani ya Yanga SC, ambako alikuwa na mchango mkubwa katika safari ya timu hiyo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita. Katika mchezo muhimu dhidi ya CR Belouizdad, Guede alifunga bao la mwisho katika ushindi wa mabao 4-0, ushindi ulioweka historia kwa Yanga.

Hata hivyo, akiwa Singida, alishindwa kufunga bao lolote kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, akifanikiwa tu kutoa pasi moja ya bao. Alipoulizwa kuhusu maamuzi ya kuvunja mkataba wake, alisema:

“Nimeitumikia Singida kwa miezi sita, hivyo, bado nilikuwa na mkataba wa miezi mingine sita ili kuumaliza lakini mara baada ya kuitwa mezani tulikubaliana kuvunja mkataba.”

Changamoto na Maoni Kuhusu Soka la Tanzania

Licha ya changamoto za majeraha na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha Singida, Guede alieleza kufurahishwa na mapenzi ya Watanzania kwa mpira wa miguu. Alisema:

“Tanzania wanapenda sana mpira na wana upendo lakini mambo ya ndani ya uwanja yana changamoto nyingi ambazo zinahitaji ukomavu ili uweze kustahimili na kuweza kuendana na kasi ya ushindani iliyopo.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kagera Sugar Karibu Kumsajili Adam Adam Kutoka Azam FC
  2. Banda Avunja Mkataba na Baroka FC Baada ya Miezi 3 Tu
  3. Winga wa Zamani wa Simba Yusuph Mhilu Atamani Kurejea Ligi Kuu
  4. Dube Afunga Goli 3 na Kuipa Yanga Ushindi Dhidi ya Mashujaa
  5. Washindi wa Tuzo za CAF 2024 (CAF AWARDS 2024)
  6. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo