Gamondi Asifu Ubora Waliouonesha Simba Kariakoo Derby

Gamondi Aweka Wazi Nia Yake ya Kutwaa Ubingwa wa Afrika

Gamondi Asifu Ubora Waliouonesha Simba Kariakoo Derby

Katika mchezo wa Derby ya Kariakoo uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, alisifu ubora wa Simba licha ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Gamondi alielezea mbinu zake za kiufundi ambazo zilipelekea Yanga kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC. Ushindi huo uliwafanya Yanga kuendelea na mwenendo wao mzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Simba ikipata kipigo chao cha kwanza msimu huu.

Gamondi alifichua kuwa mbinu yake kuu ilikuwa ni kushambulia kupitia pembeni, hasa dakika 30 za mwisho za mchezo. Alieleza kuwa alifahamu mabeki wa Simba, kama Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, hujichosha kwenye kipindi cha pili, hivyo akaamua kuwaingiza Clement Mzize na Kennedy Musonda ili kutumia nafasi zilizokuwa zinaachwa wazi. Alisema:

“Kipindi cha pili niliwaingiza Mzize na Musonda ili wakimbie kwenye nafasi za wazi. Tunafahamu Simba wanashambulia sana kupitia mabeki wao wa pembeni na dakika 30 za mwisho wanachoka na kuacha nafasi kila mechi. Huo ndio ulikuwa mpango wetu.”

Aidha, aliongeza kuwa Simba kwa kawaida hushambulia sana dakika 15 hadi 20 za mwanzo, lakini Yanga walijipanga kucheza kwa utulivu zaidi kipindi cha pili, jambo ambalo lilizaa matunda na kuwapa ushindi huo muhimu. Licha ya ushindi, Gamondi aliwapongeza Simba kwa kuimarika kwa mbinu na kuwa timu tishio.

Gamondi Asifu Ubora Waliouonesha Simba Kariakoo Derby

Fadlu Davids Atoa Lawama

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, aliilalamikia sana kazi ya mwamuzi Ramadhani Kayoko kwa kutowapa penalti katika matukio mawili ya wazi ambayo wachezaji wake walifanyiwa madhambi, hasa Kibu Denis. Fadlu alieleza kuwa mwamuzi hakutenda haki katika maamuzi yake, lakini pia alisifu kikosi chake kuwa kipo katika mchakato wa kuimarika zaidi.

Alisema, “Si kwamba Yanga ni bora kuliko sisi, bali wana uzoefu zaidi. Tunapaswa kuimarisha kikosi chetu na tunafahamu dirisha dogo lipo jirani, hivyo tutaboresha zaidi kwa kuwa mbio za ubingwa bado zipo wazi.”

Fadlu alibainisha kuwa licha ya Simba kupoteza mchezo huo, timu yake inaendelea kupata muunganiko mzuri na uzoefu ambao unawafanya kuimarika zaidi. Aliendelea kusema kwamba Yanga wanazidiwa tu kwa uzoefu, lakini Simba bado wapo kwenye mbio za ubingwa.

Yanga Wazidi Kuimarika

Bao pekee la mchezo lilipatikana dakika nne kabla ya mechi kumalizika, baada ya Kelvin Kijili wa Simba kujifunga akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na Maxi Nzengeli. Matokeo hayo yaliifanya Yanga kufikisha pointi 15 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, nyuma ya Singida Black Stars wenye pointi 16.

Yanga pia waliendelea kuweka rekodi nzuri ya kucheza michezo mitano bila kupoteza, huku wakishinda yote bila kuruhusu bao lolote. Kwa upande wa Simba, kipigo hicho kiliwashusha hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 13.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ligi Kuu Zanzibar 2024/2025 Yaanza Kuchangamka
  2. Erik Ten Hag Hajaridhika na Ushindi Dhidi ya Brentford, Ajiandaa Kukabiliana na Mourinho
  3. Ngorongoro Heroes Yatwaa Kombe la CECAFA U-20 Baada ya Kuicharaza Kenya
  4. Yanga Yaendelea Kugawa Dozi Kwa Maasimu Wake wa Msimbazi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo