Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam

Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam

Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam

Kiungo wa klabu ya Azam FC, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, amefunguka kwa kina kuhusu umuhimu wa mechi sita zilizobaki kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu huu.

Ametoa kauli hiyo baada ya ushindi wa bao 2-0 walioupata dhidi ya Ken Gold jijini Mbeya, ushindi uliowaweka Azam katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 51, zikiwa zimebaki mechi sita tu kumaliza msimu.

Kwa sasa, Young Africans SC (Yanga) ndiyo vinara wa ligi kwa alama 61 baada ya mechi 23, wakifuatwa kwa karibu na Simba SC wenye pointi 57 kutokana na mechi 22. Hali hii inaonesha wazi kuwa ushindani wa ubingwa wa ligi msimu huu ni mkali, na kila pointi inayosalia ni ya muhimu sana.

Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam

Vita ya Pointi Tatu: Mechi Kufa na Kupona

Akizungumza baada ya mechi dhidi ya Ken Gold, Fei Toto amesema kuwa mechi zote sita zilizobaki kwa Azam ni fursa ya kupambana hadi mwisho, kwani lolote linaweza kutokea katika mbio za ubingwa.

“Ushindani ni mkali kwenye ligi, lakini tunashukuru kila mmoja kikosini anapambana kadri ya uwezo wake, hatukati tamaa wala kubweteka badala yake tunatafuta pointi tatu kila mechi,” alisema Fei Toto.

Kulingana na ratiba ya Azam FC, mechi zilizobaki ni dhidi ya Singida BS (ugenini), Yanga (nyumbani), Kagera Sugar (ugenini), Dodoma Jiji (nyumbani), Tabora United (ugenini), na Fountain Gate (ugenini). Hii inaonesha kuwa Azam watakabiliana na wapinzani wa aina tofauti, huku michezo mitano kati ya sita ikichezwa nje ya uwanja wao wa nyumbani.

Fei Toto alieleza kuwa siri ya mafanikio ya Azam FC hadi sasa ni mshikamano wa wachezaji na kufuata kwa umakini maelekezo ya benchi la ufundi. Ameeleza kuwa kila mchezaji anajituma kuhakikisha timu inapata pointi tatu katika kila mechi.

Aidha, kiungo huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars, amesema mafanikio ya timu hayawezi kutokana na mtu mmoja pekee. Amedokeza kuwa sababu ya yeye kutofunga mabao mengi msimu huu ni kutokana na kuamua kutoa pasi za mabao kwa wachezaji walioko katika nafasi nzuri zaidi ya kufunga.

“Ndiyo maana nikipata nafasi nikaona siko sehemu nzuri ya kufunga nampa aliye eneo zuri na timu inashinda na ndiyo lengo letu, najivunia kuwa kinara kwenye asisti za mabao,” alisema Fei Toto.

Hadi sasa, Fei Toto ana jumla ya mabao manne na ameongoza kwa kutoa pasi za mabao kwa wachezaji wenzake (asisti 12), jambo linaloonesha mchango wake mkubwa kwa timu licha ya kutoonekana sana kwenye orodha ya wafungaji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. De Bruyne Atangaza Kuondoka Man city Mwishoni Mwa Msimu
  2. Ratiba Ya Robo Fainali Crdb Bank Federation Cup 2024/2025
  3. Simba Yaianza Robo Fainali Shirikisho CAF Kwa Kichapo Cha 2-0
  4. Matokeo ya Tabora united vs Yanga Leo 02/04/2025
  5. Kikosi cha Yanga VS Tabora united Leo 02/04/2025
  6. Viingilio Mechi ya Tabora united Vs Yanga SC Leo 02/04/2025
  7. Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo