Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho

Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho

Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho

Kesho ni siku muhimu kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania, kwani timu ya Simba SC, chini ya kocha wao mpya Fadlu David, itakutana na Azam FC kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mchezo huu wa Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili. Ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana msimu huu, kila moja ikiwa chini ya kocha mpya – Simba ikiwa na Fadlu David na Azam ikiwa chini ya Rachid Taoussi.

Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho

Historia na Rekodi ya Timu

Simba SC na Azam FC zimejijengea sifa kubwa katika soka la Tanzania. Rekodi za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Simba iliwashinda Azam kwa mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya msimu uliopita, baada ya sare ya 1-1 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Ingawa matokeo ya zamani yanaweza kutoa picha, ni muhimu kutambua kuwa kila msimu una changamoto zake. Makocha wapya, mbinu mpya, na wachezaji wapya vinafanya kila mechi kuwa na ladha tofauti.

Msimu huu, timu zote zimeanza kwa kasi na hazijaruhusu bao lolote kwenye michezo ya ligi walizocheza. Hii inaashiria kwamba mechi ya kesho itakuwa yenye ushindani mkali, kwani timu zote zinahitaji kuendelea na mfululizo wao wa kutoruhusu magoli na kuimarisha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.

Maandalizi ya Mnyama Simba SC

Kocha wa Simba SC, Fadlu David, ameeleza kuwa wanaiheshimu Azam FC kutokana na kikosi chao kilichosheheni vipaji, lakini pia amesisitiza kuwa Simba imejipanga vyema kwa mchezo huu. Akizungumza na waandishi, Fadlu alieleza kuwa wamejifunza mengi kupitia mikanda ya mechi za Azam, na wamejipanga kutumia mbinu sahihi kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Tumetoka kwenye mchezo mgumu, hivyo tunachofanya kwa sasa ni mazoezi mepesi ya viungo ili wachezaji wapumzike na kuwa tayari kwa mechi inayokuja. Tunaikubali Azam kama timu yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa, lakini tunaendelea kusoma mbinu zao kupitia mikanda ya mechi zao,” alisema Fadlu.

Kuhusu uwanja, Fadlu alitambua changamoto ya kucheza kwenye nyasi bandia lakini hakutaka kuiona kama kikwazo kikubwa kwa wachezaji wake. “Nyasi bandia sio rahisi kwa wachezaji wetu, lakini tunaamini bado tuna uwezo wa kufanya vizuri,” aliongeza.

Wachezaji wa Simba nao wameonyesha nia ya dhati ya kupata ushindi kwenye mechi hii. Beki mahiri wa Simba, Shomari Kapombe, alieleza kuwa kocha wao mpya amefanikiwa kubadili kikosi kwa haraka, na sasa timu iko katika hali bora kuelekea kwenye mechi.

“Kocha amekuwa nasi kwa muda mfupi, lakini tayari ameleta mabadiliko chanya kikosini. Kila mechi tunayocheza anatufundisha kuwa na bidii zaidi na kujirekebisha kutokana na makosa ya nyuma. Tuna uhakika wa ushindi dhidi ya Azam,” alisema Kapombe.

Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, aliweka wazi kuwa wanajiamini kuelekea kwenye mechi hiyo. Aliongeza kuwa wamepata mafunzo mazuri kutoka kwa kocha wao na wamejipanga kufuata mbinu alizowaelekeza. Pia aliweka wazi kuwa wamekuwa wakitazama mikanda ya mechi za Azam ili kujua nguvu na udhaifu wa wapinzani wao.

“Malengo yetu msimu huu ni kuchukua ubingwa, na tumeanza vizuri. Tumeshinda mechi mbili bila kuruhusu bao, na tuna uhakika Azam hawawezi kuvunja rekodi yetu,” alisema Tshabalala kwa kujiamini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kengold Vs Yanga Leo 25/09/2024 Saa Ngapi
  2. Kikosi cha Yanga Vs Kengold Leo 25 September 2024
  3. JKT Tanzania VS Coastal Union Leo 25/09/2024 Saa Ngapi?
  4. Kengold Wakijichanganya Tunawapiga Nyingi, Gamondi Atoa Onyo
  5. Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba
  6. Takwimu za Chama Yanga zaanza kutisha Klabu Bingwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo