England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

Usiku wa kusisimua unakaribia katika Uwanja wa Olympiastadion, Berlin, ambapo miamba wa soka Ulaya, England na Hispania, watapambana vikali kuwania taji la mabingwa wa bara la Ulaya ijulikanayo kama EURO 2024. Mtanange huu wa fainali una historia ndefu na takwimu za kusisimua, na mashabiki wa soka kote duniani wanajiuliza. Fainali hii inaweza kua ni fursa ya Hispania kujinyakulia taji lao la nne la Ulaya, wakati Uingereza inatafuta kumaliza ukame wa miaka 58 bila taji la kimataifa. Je, ni Simba wa Uingereza watakaonguruma, ama La Roja ya Hispania watawika tena?

Safari ya England na Hispania Kuelekea Fainali ya EURO 2024

Timu zote mbili zimeonyesha kiwango cha hali juu hadi kufika fainali hii ambayo inatarajiwa kuchezeka leo hii julai 14 2024 saa nne usiku.

Hispania, wakiwa mabingwa mara tatu wa Ulaya, wamekuwa moto wa kuotea mbali, wakithibitisha ubora wa kikosi chao kilicho jaa nyota chipukizi kwa kuwatoa vigogo kama Ujerumani na Ufaransa. Lamine Yamal, kinda mwenye umri wa miaka 17 tu, amekuwa nyota angavu katika kikosi cha La Roja, akifunga na kutoa pasi za mabao kwa ustadi mkubwa.

England, kwa upande wao, wamepitia njia yenye misukosuko, wakilazimika kupambana hadi dakika za mwisho katika mechi kadhaa. Hata hivyo, ushupavu wao na ari ya kupigania ushindi umewapa tiketi ya fainali hii ya kihistoria. Harry Kane, kinara wa mabao wa Uingereza, atakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha Simba wa Uingereza wanang’oa taji lao la kwanza la Ulaya tangu mwaka 1966.

Matokeo ya Fainali ya EURO 2024 England vs Hispania

England  1-2 Hispania
  • Wafungaji Magoli Hispania; Nico Williams – 47’Mikel Oyarzabal – 86′
  • Mfungajio wa Goli la England; Cole Palmer – 73′

England vs Hispania: Matokeo ya Fainali ya EURO 2024

Historia ya England vs Hispania Michezo Iliyopita

Katika historia, England na Hispania wamekutana mara 27 katika mechi rasmi, na Uingereza wakiwa na ushindi mara 14, sare tatu, na Hispania mara 10. Hata hivyo, takwimu hizi hazitoi picha kamili. Mechi za hivi karibuni zimekuwa ngumu, na ushindi ukitawaliwa na timu moja au nyingine. Mtanange huu wa fainali, bila shaka, utakuwa na sura yake ya kipekee.

Idadi ya Michezo Waliokutana 27
Mechi Alizoshinda Hispania 10
Sare 3
Mechi Alizoshinda England 14

Matokeo ya Mechi kati ya Uingereza na Hispania

Tarehe Matokeo Mashindano
Oktoba 15, 2018 Hispania 2-3 Uingereza Ligi ya Mataifa, Awamu ya Ligi
Septemba 08, 2018 Uingereza 1-2 Hispania Ligi ya Mataifa, Awamu ya Ligi
Novemba 15, 2016 Uingereza 2-2 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 13, 2015 Hispania 2-0 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 12, 2011 Uingereza 1-0 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 11, 2009 Hispania 2-0 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 7, 2007 Uingereza 0-1 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 17, 2004 Hispania 1-0 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 28, 2001 Uingereza 3-0 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Juni 22, 1996 Uingereza 0-0 Hispania (penalti 4-2) Mashindano ya Ulaya, Robo-Fainali
Septemba 9, 1992 Hispania 1-0 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Februari 18, 1987 Hispania 2-4 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Julai 5, 1982 Hispania 0-0 Uingereza Kombe la Dunia, Awamu ya Makundi
Machi 25, 1981 Uingereza 1-2 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Juni 18, 1980 Uingereza 2-1 Hispania Mashindano ya Ulaya, Awamu ya Makundi
Machi 26, 1980 Hispania 0-2 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 8, 1968 Hispania 1-2 Uingereza Mashindano ya Ulaya, Robo-Fainali ya Mchujo
Aprili 3, 1968 Uingereza 1-0 Hispania Mashindano ya Ulaya, Robo-Fainali ya Mchujo
Mei 24, 1967 Uingereza 2-0 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Desemba 8, 1965 Hispania 0-2 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Oktoba 26, 1960 Uingereza 4-2 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Novemba 30, 1955 Uingereza 4-1 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 18, 1955 Hispania 1-1 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Julai 02, 1950 Hispania 1-0 Uingereza Kombe la Dunia la FIFA
Desemba 09, 1931 Uingereza 7-1 Hispania Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa
Mei 15, 1929 Hispania 4-3 Uingereza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa

Uchambuzi: Mbinu na Wachezaji Muhimu

Spain wanatarajiwa kuja na mbinu yao ya tiki-taka, wakipiga pasi nyingi na kutawala mpira kwa muda mrefu. Wachezaji wao mahiri, kama vile Pedri, Gavi, na Dani Olmo, watajaribu kuvuruga safu ya ulinzi ya Uingereza. Kwa upande wao, England watategemea kasi ya wachezaji kama Bukayo Saka na Raheem Sterling kushambulia kwa kushtukiza huku uzoefu na uwezo wa nyota wa england kama Harry Kane unatarajiwa kua msaada mkubwa.Pia Jude Bellingham, atakuwa na jukumu la kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Robo Fainali EURO 2024 & Ratiba
  2. Msimamo Makundi ya EURO 2024
  3. Matokeo Ya Mechi Za Euro 2024
  4. Ratiba Kamili ya UEFA Euro 2024 Hatua Ya 16 Bora
  5. Timu zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Euro 2024
  6. Wafungaji Bora EURO 2024: Hawa Ndio Vinara Wa Magoli
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo