Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora

Hatua ya 16 bora Kombe la FA

Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora | Mechi Za Hatua ya 32 & 16 Bora Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup | Droo Ya Kombe la FA Tanzania

Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025

Droo ya hatua ya 32 na 16 bora ya michuano ya CRDB Federation Cup almaarufu kama Kombe la FA Tanzania imekamilika rasmi. Kwa mujibu wa matokeo hayo ya droo, michezo ya raundi ya 32 inatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 1 hadi 4, huku mechi za hatua ya 16 bora zikitarajiwa kufanyika mwezi Aprili.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Yanga SC, wamepangwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga kwenye raundi ya 32, huku watani wao wa jadi, Simba SC, wakipewa TMA Stars inayoshiriki Ligi ya Championship. Klabu ya Azam FC nayo imepangwa kuvaana na Mbeya City katika hatua hii ya awali.

Droo hii ilichezeshwa makao makuu ya Azam TV, Tabata jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Meneja Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto.

Mechi Zitakazo Tazamwa Zaidi Na Mashabiki

Katika droo hii, kuna michezo kadhaa ambayo bila shaka itavutia hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, ikiwa ni pamoja na:

  1. Yanga SC vs Coastal Union – Huu ni marudio ya fainali ya mwaka 2022, ambapo timu hizi zilitoka sare ya mabao 3-3 kabla ya Yanga kushinda kwa penalti 4-1.
  2. Simba SC vs TMA Stars – Simba SC inapambana na timu yenye rekodi nzuri katika Championship msimu huu.
  3. Azam FC vs Mbeya City – Azam italazimika kuwa makini dhidi ya wapinzani wao kutoka Mbeya.
  4. Polisi Tanzania vs Songea FC – Mchezo wa timu mbili zenye uzoefu katika michuano hii.
  5. Kagera Sugar vs Namungo FC – Timu zote zinajulikana kwa ushindani mkubwa kwenye Kombe la FA.

Mechi za Hatua ya 32 Bora Kombe La Shirikisho la CRDB: Ratiba Kamili

  • Cosmopolitan FC vs KMC FC
  • Mbeya Kwanza vs Mambali Academy
  • Tanzania Prisons vs Big Man
  • Kagera Sugar vs Namungo
  • Polisi Tanzania vs Songea United
  • Kiluvya Utd vs Pamba Jiji FC
  • Mtibwa Sugar vs Towns Stars
  • Giraffe Academy vs Green Warriors
  • JKT Tanzania vs Biashara Utd
  • Tabora Utd vs Transit Camp
  • Mashujaa FC vs Geita Gold
  • Simba SC vs TMA Stars
  • Azam FC vs Mbeya City
  • Singida BS vs Leo Tena
  • Yanga SC vs Coastal Union
  • Fountain Gate vs Stand Utd

Droo ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025 Hatua ya 32 & 16 Bora

Mechi Za Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup: Ratiba Kamili

  • Tabora Utd/Transit Camp vs Kagera Sugar/Namungo FC
  • Mashujaa FC/Geita Gold vs Kiluvya Utd/Pamba Jiji FC
  • Fountain Gate/Stand Utd vs Giraffe Academy/Green Warriors
  • Yanga SC/Coastal Union vs Polisi Tanzania/Songea FC
  • Singida BS/Leo Tena vs Cosmopolitan FC/KMC FC
  • JKT Tanzania/Biashara Utd vs Mbeya Kwanza/Mambali Academy
  • Azam FC/Mbeya City vs Mtibwa Sugar/Towns Stars
  • Simba SC/TMA Stars vs Tanzania Prisons/Big Man

Mechi Za Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup

Mchakato wa Michuano na Fainali

Kwa mujibu wa Baraka Kizuguto, bado kuna mchakato wa kutafuta uwanja utakaochezwa fainali ya Kombe la FA msimu huu. TFF inaendelea kupokea maombi kutoka mikoa mbalimbali ili kuamua mahali ambapo mchezo huo wa kihistoria utafanyika. Mashabiki wa soka wanatarajia kuona mechi kali na za kusisimua katika hatua hizi mbili za michuano. Timu zitakuwa zinapambana sio tu kwa ajili ya kutwaa taji, bali pia kwa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu ujao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
  2. Kikosi cha Simba vs Fountain Gate Leo 06 Februari 2025
  3. Fountain Gate VS Simba Leo 06 Februari 2025 Saa Ngapi?
  4. RATIBA ya Mechi za Leo 06 Februari 2025
  5. CV ya Miloud Hamdi, Kocha Mpya wa Yanga 2025
  6. Matokeo ya Yanga vs Kengold Leo 05/02/2025
  7. Kilichomuondoa Ramovic Yanga Hatimaye Chafichuka
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo