DR Congo Vs Tanzania Taifa stars Leo 10/10/2024 Saa Ngapi?

DR Congo Vs Tanzania Taifa stars Leo 10 10 2024 Saa Ngapi

DR Congo Vs Tanzania Taifa stars Leo 10/10/2024 Saa Ngapi?

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, almaarufu kama Taifa Stars, leo itakuwa mgeni wa DR Congo katika mchezo muhimu wa Kundi H wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mtanange huu unatarajiwa kuwa mkali na wenye mvuto wa aina yake, huku kila timu ikitafuta ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali zitakazofanyika Morocco.

Taifa Stars wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wao uliopita. Ushindi huu umewapa ari na kujiamini, na wachezaji wameapa kupambana ili kupata matokeo mazuri dhidi ya DR Congo. Hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto kubwa kwani DR Congo wanaongoza kundi hili wakiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zao zote mbili za awali.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ya upinzani mkali kutokana na historia ya michezo kati ya timu hizi mbili.

Katika miaka ya hivi karibuni, DR Congo imekuwa tishio kwa Taifa Stars, ikiwa imeshinda mara mbili na kutoka sare mara tatu katika mechi sita zilizopita. Hata hivyo, Taifa Stars wanaamini kuwa wanaweza kugeuza matokeo na kuandika historia mpya leo.

Wataalamu wa soka wanabashiri mchezo mgumu na wenye ushindani mkali, huku wakisisitiza umuhimu wa nidhamu, umakini, na utumiaji mzuri wa nafasi kwa Taifa Stars ili kuibuka na ushindi. Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya TV na Radio ili kuwapa sapoti Taifa Stars.

Muda wa Mechi ya DR Congo Vs Tanzania Taifa stars Leo 10/10/2024

DR Congo Vs Tanzania Taifa stars Leo 10/10/2024 Saa Ngapi?

Mechi hii itachezwa saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa wale ambao hawataweza kufika uwanjani, mechi itarushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya televisheni ikiwemo Azam Tv. Endelea kufuatilia matangazo ili kujua ni wapi utaweza kuitazama.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Cole Palmer Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwaka 2023/24
  2. Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA
  3. Ratiba Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2024/2025
  4. Chama- Ndoto ya Ubingwa wa Afrika na Yanga Inawezekana!
  5. Kikao Cha Masaa Saba Man Utd Chamalizika Bila Taarifa ya Hatma ya Ten Hag
  6. Timu 5 Zinazopewa Nafasi Kubwa Kushindwa Klabu Bingwa Ulaya 2024/2025
  7. Andres Iniesta Atundika Daluga Baada ya Miaka 22 Ndani ya Soka la Kulipwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo