Dickson Job: Fedha za Goli la Mama Zinatupandisha Morali

Fedha za Goli la Mama zinatupandisha Morali

Dickson Job: Fedha za Goli la Mama zinatupandisha Morali

Beki wa kati wa Yanga, Dickson Job, amefunguka kuhusu hamasa kubwa wanayoipata kutokana na ahadi ya fedha inayotolewa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kila goli wanalofunga.

Katika mashindano ya kimataifa wanayoshiriki, timu ya Yanga imekuwa ikipata matokeo mazuri, jambo ambalo Job anasema linachangiwa kwa kiasi kikubwa na motisha inayotolewa na Rais Samia. Job alikuwa nahodha kwenye mchezo wa juzi dhidi ya timu ya CBE ya Ethiopia, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Dickson Job: Fedha za Goli la Mama zinatupandisha Morali

Akizungumza baada ya mechi, Job alieleza kuwa kila mchezaji amekuwa akijitolea zaidi uwanjani kutokana na ahadi ya fedha zinazotolewa na Rais Samia kwa kila goli wanalofunga.

“Ni kweli kabisa ushindi huu na hata mechi zilizopita, pesa za mama yetu zimekuwa zikitupa hamasa sana,” alieleza Job. “Tunapopata goli, fedha hutolewa na tunagawana wachezaji, jambo ambalo linatupa motisha ya kucheza kwa nguvu zaidi ili tushinde na kupata mabao mengi.”

Motisha hii ya kifedha inawasaidia wachezaji wa Yanga kuongeza jitihada zao uwanjani, huku wakiweka nguvu kubwa kuhakikisha wanashinda michezo yao kwa kishindo. Ushindi huo sio tu unaleta furaha kwa wachezaji, bali pia unawapa mashabiki wa Yanga furaha kubwa. Hii imekuwa ni mbinu ya kuongeza morali na kupandisha ari ya ushindi katika mashindano ya kimataifa.

Mbinu za Kocha na Nguvu za Kikosi

Kuhusu mchezo wa juzi, Job alieleza changamoto walizokutana nazo katika kipindi cha kwanza. Alisema wapinzani wao walijikita zaidi katika kujilinda kwenye eneo lao, jambo lililowafanya Yanga kushindwa kufunga mabao mengi mwanzoni mwa mchezo. “Kipindi cha kwanza wapinzani walikuwa na wachezaji wengi nyuma, hivyo ilitulazimu kutumia mbinu za kiufundi kufikia goli lao,” alieleza Job.

Hata hivyo, baada ya mapumziko, kocha aliwapa maelekezo maalum na waliporejea uwanjani, walibadilika na kuanza kwa kasi. Ndani ya dakika chache za kipindi cha pili, walifanikiwa kupata bao la pili, na kisha kuendelea kuwabana wapinzani hadi kupata mabao mengine matano.

Job pia aliwapongeza wachezaji wa Yanga kwa juhudi zao, hasa wale ambao walipata nafasi ya kucheza huku wengine wakikosekana. Alisema, “Kikosi chetu kina upana wa kutosha, kila mchezaji anapewa nafasi anaonesha kiwango bora. Hata wachezaji wa kikosi cha kwanza walipokosekana, wale waliopata nafasi walifanya kile ambacho mwalimu anataka.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Gamondi Asema Hakuna wa Kumtisha Makundi Klabu Bingwa
  2. Haaland Afikisha Magoli 100 Man City, Aifikia Rekodi ya Ronaldo
  3. Simba Yafuzu Makundi Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  4. Kocha wa Yanga Aeleza sababu ya kumpiga benchi Dube
  5. Kelvin John Bado Kidogo Taifa Stars
  6. KenGold Yajipanga Kutingisha Nyavu za Yanga SC Ligi Kuu
  7. Guardiola Atoa Tamko Kali: Wapinzani ‘Wana Roho Mbaya’
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo